Loading...
title : BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI
link : BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI
BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
BWENI la wavulana katika Shule ya Sekondari Mlangarini ambayo ni shule ya Serikali iliyo katika kata Mlangarini Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru limeungua moto.
Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro amesema leo Januari 12,2019 amepata taarifa za kuungua kwa bweni saa moja asubuhi.
Amesema taarifa za awali zinaeleza moto huo ulianza Alfajiri na kuteketeza chumba kimoja kati ya vyumba 14 vya bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 84 na kwamba hakuna majeruhi wala vifo.
"Japo kuna uharibifu wa mali ikiwemo kuungua kwa vitanda (double) vitatu (3),magodoro (6),Masanduku ya kuhifadhia nguo na madaftari. Kutokana na changamoto hiyo nililazimika kufika eneo la tukio mapema na kuungana na wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika hatua za awali ambapo pia kikosi cha Zimamoto kiliwahi kufika kwenye eneo la tukio na kukuta moto umezimwa kwa ( fire extinguisher 11)," amesema Muro.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro akizungumza jambo mbele ya baadhi ya waalimu wa shule hiyo pamoja na majirani wanaoinzunguka shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro akimsikiliza mmoja wa Waalimu wa shule hiyo mara baada ya tukio
Moja ya chumba kilichoteketea moto
Hivyo makala BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI
yaani makala yote BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/bweni-la-shule-ya-sekondari-mlangarini.html
0 Response to "BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI"
Post a Comment