Loading...
title : CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA.
link : CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA.
CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili kutoa maoni kuhusu muswada wa sheria wa vyama vya siasa.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili kutoa maoni kuhusu muswada wa sheria wa vyama vya siasa.
Mkutano huo umewakutanisha wanachama wa CCM pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani kwa Lengo la kujadili na kutoa maoni kwa ajili ya kuboresha muswada wa sheria za vyama vya siasa.
Akizungumza katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema kuwa ni vizuri tukatoa maoni yetu katika muswada huo ambao ni muhimu katika vyama vya siasa hapa nchini.
Polepole amesema kuwa kuna mambo ambayo yamekuwa yakifanyika ambayo sio rafiki katika vyama vya siasa jambo ambalo limekuwa ni changamoto kwa msajili wa vyama vya siasa kutekeleza majukumu yake.
Amesema kuwa naamini kupitia mkutano huo kila mtu atatoa maoni yake katika kuhakikisha sheria hiyo inaboreshwa.
"Sheria hii iwe nzuri au mbaya tuna haki ya kutoa maoni ili tupate sheria ambayo ni bora" amesema Mhe. Polepole.
Ameeleza kuwa kuna vyama vya siasa vimekuwa vikitumia fedha za ruzuku kinyume na utaratibu, hivyo kupitia muswada fedha za umma zitatumika kama zilivyokusudiwa.
Hata hivyo amewataka wanachama wa CCM na wadau wa siasa kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria wa vyama vya siasa ambao ni rafiki kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Hivyo makala CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA.
yaani makala yote CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/ccm-yakutana-dar-kujadili-muswada-wa.html
0 Response to "CCM YAKUTANA DAR KUJADILI MUSWADA WA SHERIA VYAMA VYA SIASA."
Post a Comment