Loading...
title : DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5
link : DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5
DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5
Mkuu wa wilaya ya Ilala sophia Mjema akiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Togo ,Shule ya MSINGI Gogo Kata ya Zingiziwa Wilayani Ilala wakati wa kukata utepe katika uzinduzi wa Ofisi ya Walimu na madarasa matatu yaliojengwa Kwa msaada wa Serikali ya Japan yaliogharimu dola za Marekani 94.5,(Kushoto) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri (Kulia) Ofisa Elimu Msingi Manispaa hiyo Elizabeth Thomas (PICHA NA HERI SHAABAN)
Balozi wa Japan nchinï Tanzania Shinichi Togo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Gogo Kata ya Zingiziwa Wilayani Ilala Dar es Salam jana wakati wa kupokea msaada wa madarasa matatu na ofisi ya Walimu yaliojengwa Kwa msaada wa Serikali ya Japan (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mwambawahabari
Na Heri Shaban
MKUU wa wilaya ya Ilala sophia Mjema amekabidhiwa jengo la ofisi ya Walimu lenye thamani ya dola za Marekani 94.5 kutoka Serikali ya watu wa Japan pamoja na madarasa matatu Kwa ajili ya Shule ya Msingi Gogo iliopo Zingiziwa Wilayani Ilala.
Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salam jana ambapo Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto alimbidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala.
Akipokea msaada huo wa jengo la Utawala Shule ya Gogo Sophia Mjema alipongeza Serikali ya Japan kwa Ushirikiano wao kusaidia kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli za kutoa elimu ya Msingi bila ya malipo inayokwenda sambamba na kuboresha miundombinu ya Elimu nchini.
"Katika shule hii ya Gogo MANISPAA ILALA tutatoa Wataalam wa kisasa wa Sayansi, waje endesha ndege ,na Wahandisi watatoka katika shule hii kwani ujenzi huo umekuja wakati mzuri katika shule za Serikali Manispaa ya Ilala matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 Mwanafunzi wa kwanza pia ametoka shule hiyo " alisema Mjema.
Mjema alisema Mradi huo unatarajia kuwa na faida kubwa mfano kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani, kupunguza utoro Kwa wanafunzi, umeboresha MAZINGIRA ya kufundishia na kujifunza pia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi Mradi huo utazidi kuimarisha mahusiano mema kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan.
Aliwataka wanafunzi wa Manispaa ya Ilala kuzingatia masomo ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Kwa upande wake Mkurungezi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema Mradi wa upanuzi wa Shule hiyo ulianza Mei 2018 Kwa ufadhili wa Serikali Japan Halmashauri pamoja na Jamii, utekelezaji wa Mradi huo umehusisha, ujenzi wa jengo la Utawala, vyumba vitatu vya madarasa pamoja na thamani za ofisi,kalo la maji taka.
" Shule hii ina wanafunzi 2366 kati yake Wavulana 1202 na
Wasichana 1164 gharama ya Mradi 208,919,700 kati ya fedha hizo Serikali ya Japan imetoa dola za Marekani 94.5.sawa na.shilingi 204,790,806 na Halmashauri ya Ilala ilichangia shilingi 4,128,894 " alisema Shauri.
Alisema Halmashauri ya Ilala itakikisha inatunza vyumba vya darasa, jengo la Utawala pamoja na thamani ya ofisini ili kuakikisha zinakuwa endelevu zitumike mda Mirefu " alisema Shauri.
Naye Balozi wa Japani Nchini Tanzania Shinichi Goto alisema Mradi huo utasaidia kutoa MAZINGIRA mazuri ya kusoma pamoja na kufundishia ambapo Shule hiyo itakuwa mfano Kwa Shule zingine.
Balozii Goto aliwakikishia kwamba Serikali ya Japan itaendelea kusaidia Maendeleo ya nchi yetu na ILALA kwa ujumla tukio hilo ni hatua nyingine kubwa katika kuimalisha ushirikiano mzuri baina nchi hizo mbili Japan na Tanzania.
Hivyo makala DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5
yaani makala yote DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/dc-mjema-apokea-jengo-la-ofisi-ya.html
0 Response to "DC MJEMA apokea jengo la Ofisi ya Walimu kutoka Serikali ya Japan lenye thamani ya Dola za Marekani 94.5"
Post a Comment