Loading...
title : DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI
link : DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI
DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI
Na Mwandishi Wetu Mbinga
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka jamii kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu ili kuwa na Jamii yenye mabinti wasomi na kuondokana na ukandamizaji wa watoto wa kike na wanawake.
Dkt. Ndugulile ametoa rai hiyo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati akishirikiana na wananchi katika ujenzi wa Bweni la shule ya Sekondari Mikalanga ambalo kwa kiasi kikubwa wananchi wametoa nguvu zao katika kufanikisha ujenzi huo.
Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa suala la elimu kwa mtoto wa kike na muhimu kutokana na changamoto za mtoto wa kike hasa suala la mimba za utotoni ambazo zinapelekea kupotea kwa ndoto za wanafunzi wa kike wengi.
Naibu Waziri Ndugulile amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo Mtoto mmoja kati ya watoto watatu wa kike hupata mimba za utotoni na kukatisha ndoto za Mtoto wa kike kupata elimu kati ya miaka 15 mpaka 19 ikiwa sawa na asilima 27.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwasili katika shule ya Sekondari Mikalanga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Cosmas Nshenye na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani kwenda kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa bweni la wasichana shuleni hapo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia kikundi cha ngoma za asili katika shule ya Sekondari Mikalanga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Cosmas Nshenye na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani kwenda kushirikiana na wanachi katika ujenzi wa bweni la wasichana shuleni hapo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akishirikiana na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani katika ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mikalanga.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi waliojitokeza kushirki katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Mikalanga ikiwa ni juhudi za wananchi kupunguza adha ya watoto wa kike kupata mimba shuleni.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi mmoja ya mifuko 50 aliyochangia katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mikalanga ikiwa ni juhudi za wananchi kupunguza adha ya watoto wa kike kupata mimba shuleni.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI
yaani makala yote DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/dktndugulile-tunataka-taifa-la-mabinti.html
0 Response to "DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI"
Post a Comment