Loading...

HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA

Loading...
HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA
link : HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA

soma pia


HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA

NA WAMJW-GEITA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Hospitali ya mkoa wa Geita kuhakikisha wanafungua duka la dawa ili kutoa huduma karibu na wananchi pia kuongeza mapato ya Hospitali.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo mapema leo wakati alipoitembelea hospitali hiyo ili kuona hali ya miundombinu pamoja na utoaji wa huduma za afya.
“Tumeshaagiza Hospitali zote nchi nzima kuwa na maduka ya dawa ya Hospitali, kwanini hapa hamjafungua duka lenu? Alihoji Waziri Ummy na kuongeza “sasa nawapa miezi miwili uongozi wa Hospitali kuhakikisha mnafungua duka la dawa la Hospitali ili liweze kuwasaidia kupandisha mapato lakini pia kusogeza huduma karibu na wananchi. Alisema Waziri huyo.

Pamoja na hayo Waziri Ummy ameonekana kuridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa wa zaidi ya asilimia 90 na uboreshwaji wa huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali hiyo.Kabla ya hapo Waziri Ummy alitembelea ujenzi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita ambapo alishuhudia ujenzi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 54 lakini amemtaka mkandarasi anayesimamia ujenzi huo ambaye ni wakala wa ujenzi (TBA) kufanya kazi usiku na mchana ili Hospitali hiyo ianze kufanya kazi ifikapo Mwezi Julai 2019.

Waziri Ummy amekamilisha ziara yake ya mkoa wa Geita kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Chato ili kujiridhisha na hali ya utoaji wa huduma za afya na miundombinu pamoja na kuhakikisha kama vifaa na vifaa tiba vinapatikana Hospitalini hapo.

Waziri Ummy ameridhishwa na utolewaji wa huduma za afya lakini ameitaka Hospitali hiyo kuwa na chumba maalum chenye vifaa maalum vya uangalizi wa watoto wachanga mahututi na wale waliozaliwa kabla ya siku (watoto njiti) lengo likiwa ni kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini.

Aidha, waziri huyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuanzisha kitengo cha huduma za wagonjwa wa dharura na wale waliopata ajali ikiwa ni agizo la serikali kwa hospitali zote za wilaya na mikoa nchi nzima.Huo ni muendelezo wa ziara za Waziri Ummy katika mikoa ya kanda ya ziwa kutembelea Hospitali mbalimbali kuangalia hali ya miundombinu na utoaji wa huduma za afya.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongozana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita Bw. Josephat Maganga (kulia) wakitoka kukagua jengo la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia mashine mpya ya X-ray ya kidigitali iliyifungwa katika Hospitali ya wilaya ya Chato wakati alipoitembelea hospitali hiyo kuona hali ya utoaji huduma za afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia ramani ya majengo za majengo ya Hospitali ya rufaa ya Geita wakati alipotembelea ujenzi huo. Pembeni ni msimamizi wa ujenzi huo Injinia Grace Elias.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyekuja kupata matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Geita. Katikati ni mama wa mtoto huyo Bi. Jenista Benedicto.



Hivyo makala HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA

yaani makala yote HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/hospitali-mkoa-wa-geita-yapewa-siku-60.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "HOSPITALI MKOA WA GEITA YAPEWA SIKU 60 KUFUNGUA DUKA LA DAWA"

Post a Comment

Loading...