Loading...
title : HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA
link : HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA
HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA
Na Ripota Wetu
INASIKITISHA !Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea tukio la kushambuliwa kwa Hoteli ya kifahari ya DusitD2 nchini Kenya.
Tukio la kushambuliwa kwa hoteli hiyo iliyopo eneo la 14 Riverside Nairobi nchini Kenya limetokea leo Januari 15,2019.Shambulio hilo limeibua hofu na taharuki kwa wananchi walio wengi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa wakati wa shambulio ilisikika milipuko na milio ya risasi katika eneo la hoteli hiyo na kwamba kuna milio mikubwa miwili isikika kwa kishindo kikubwa.
Kutokana na shambulio hilo la mlipuko inaelezwa watu kadha wamejeruhiwa ambapo maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu waliamua kutoa msaada kwa kushirikiana na watu wengine waliokuwa eneo hilo baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Mwandishi wa BBC ambaye yupo eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea mchana wa saa saba, Fredinand Omondi anaripoti kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa kikosi maalumu cha Recce squad kimewasili eneo la tukio ili kuongeza nguvu ya uokozi wa raia na kupambana na wavamizi.
Pia Omondi pia anaripoti kuwa moja ya maofisa usalama waliopo eneo la tukio amemwambia "hali sio nzuri".Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Kenya linaelezwa kuwa limeimarisha ulinzi eneo hilo huku wakiamua kuweka katazo la watu na magari kupita eneo ambalo limeshambuliwa.

Hivyo makala HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA
yaani makala yote HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/hoteli-ya-kifahari-yashambuliwa-kenya.html
0 Response to "HOTELI YA KIFAHARI YASHAMBULIWA KENYA, HOFU YATANDA KWA WANANCHI KILA KONA"
Post a Comment