Loading...
title : KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA
link : KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA
KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha kwa lengo la kuendelea kuwakumbusha kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo juu ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na uporaji n.k.
Aidha aliainisha madhara ya utakasishaji wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara hayo pamoja na uhalifu kuendelea kushamiri kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi; kuhatarisha utawala wa sheria na usalama (threaten peace, stability and rule of law) kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti vyombo vya au kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani (ruin competitiveness) wa kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na fedha haramu, wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha hadhi ya nchi kimataifa (erosion of country’s integrity) na kusababisha nchi kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa; kushusha imani ya wawekezaji na kusababisha uwekezaji kupungua na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na nchi huathirika kiuchumi; kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha; na nchi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya nchi.
Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu amewaasa na kuwakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria kwa uadilifu na uaminifu ili kuendelea kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi.
Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka benki na taasisi zinazotoa huduma za kibenki na huduma ndogo ndogo za fedha.
Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini.
Kamishna Msaidizi, Huduma za Kompyuta Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Gilbert .R.Nyombi akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini alipokuwa akitoa mada juu ya kudhibiti fedha haramu.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Mtaalamu kutoka FIU Bw. Girbert R. Nyombi.
Washiriki wakiwa katika Makundi kujadili mada zilizowashirishwa na wao kuchangia katika suala zima la utakatishaji fedha kutumia tasisi za kifedha.
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe
Hivyo makala KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA
yaani makala yote KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/kamishna-wa-fiu-awapa-somo-watumishi-wa.html
0 Response to "KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA"
Post a Comment