Loading...
title : KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA
link : KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA
KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mnamo Januari 11,Magufuli Mh. Aweso ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze ambapo mradi huo tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.
Kisha Mh. Aweso ameendelea na Ziara hiyo katika kata ya Kibirizi ambapo ameweza kuzindua Mradi mpya wa Maji wenye zaidi ya Shilingi Milioni 500. Mradi huo uliopo katika Kijiji cha Kibirizi umeanza kuhudumia takribani vitongoji 10 kati ya 14 vinavyopatikana ndani ya Kijiji hicho na huku juhudi zikiendelea kufanyika kuwafikia wananchi wengine.
Kwa upande mwingine mradi wa Maji Kijiji cha Kyamulalile na Mashule kwa sasa haufanyi kazi kutokana na athali ya tetemeko licha ya kuwa tayari Halmashauri imekwishatenga zaidi ya shilingi milioni 80, kwa ajili ya Ukarabati na tayari mkandarasi ameanza upembuzi yakinifu.
Naibu Waziri Aweso ameendelea kuwaomba wananchi kutunza na kulinda miradi hiyo, huku pongezi nyingi zikimmiminikia Mh. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake jinsi anavyoendelea kupambana na adha hii ya Maji, na sasa akina asilimia kubwa ya akinamama hawatembei tena mwendo mrefu kufuata Maji na kampeni ya kuwatua Ndoo vichwani inaendelea.
Pichani kati ni Naibu Waziri wa Maji Mh.Jumaa Aweso akiwa na baadhi akibeba ndoo kichwani kuashiria uzinduzi wa Maji katika Kijiji cha Kibirizi, Halmashauri ya Bukoba,ambapo pia ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni ya kumtua Mama Ndoo ikiendelea kutekelezwa mkoani Kagera.Mh.Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
Pichani jiwe la msingi Kijiji Kibiri
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akitoka kuzindua mradi wa maji kijiji cha Kibirizi,Bukoba mkoani Kagera,Mh Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ,ambapo pia ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze,ambao tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.
Hivyo makala KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA
yaani makala yote KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/kampeni-ya-kumtua-mama-ndoo-inaendelea.html
0 Response to "KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA"
Post a Comment