Loading...
title : MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO.
link : MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO.
MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO.
Na Abdullatif Yunus - Kagera
Kutokana na ukosefu wa huduma ya Maji katika baadhi ya maeneo Nchini, ambayo miradi ya Maji kuharibiwa na kuhujumiwa na Majangili wa miundo mbinu ya Maji, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza Viongozi kuweka Ulinzi madhubuti kwa ajili ya kulinda wahujumu hao na pindi watakapobainika sheria ifuate mkondo wake.
Akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani Ngara jana Januari 12,2019, Naibu Waziri Aweso amesema Serikali imekuwa ikiwekeza pesa nyingi kwa miradi mbalimbali ya Maji hapa Nchini, lakini miundo mbinu ya miradi hiyo imekuwa ikiharibiwa na wakati mwingine kuibwa na wale alowaita Majangili wa Maji.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Aweso ametembelea mradi wa Maji unaosukumwa kwa Nishati ya Umeme unaohudumia Vijiji vya Muhweza na Murugarama. Mradi huo Ulioanza Mwaka 2014, ni miongoni mwa Vijiji 10 chini ya programu ya Sekta ya Maji (WSDP) wenye gharama zaidi ya Shilingi Milioni 559.
Pichani ni Mtoto Zainabu Mohammed Mkazi wa Muhweza akisuuza Ndoo kabla ya Maji kama alivyokutwa na Kamera yetu.
Pichani ni Bi. Zubeda Baraka Mkazi wa Muhweza Wilayani Ngara, akifurahia huduma ya Maji iliyosogezwa karibu baada ya kuteseka kwa muda kufuata Maji umbali mrefu.
Tanki la Maji la Mradi wa Vijiji vya Muhweza na Murugarama unaoendelea kujengwa na Unatarajiwa kuzinduliwa Machi mwaka huu unaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 559.
Pichani Mh. Aweso akiwa juu ya Tanki la Maji linaloendelea kujengwa likiwa katika hatua za mwisho licha ya kuanza kuhudumia mradi huo.
Mh. Aweso Naibu Waziri wa Maji akinawa mkono katika Tanki kwenye mradi wa Maji wa Muhweza - Murugarama alipotembelea mradi huo mapema Januari 12, 2019.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso (MB) akishiriki kazi ya kutandaza mabomba ya maji katika mradi huo unaotekelezwa katika vijiji vya Kabalenzi-Kanazi
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na Kaimu Mhandisi wa Wilaya ya Ngara, Simon Ndyamukama kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kabalenzi-Kanazi.
Hivyo makala MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO.
yaani makala yote MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/majangili-wanaohujumu-miundombinu-ya.html
0 Response to "MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO."
Post a Comment