Loading...
title : Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika
link : Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika
Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika

Waafrika milioni 400 wanatumia intaneti.
Mahitaji ya Waafrika ni sawa na kwingineko duniani kote. Wanahitaji bidhaa nzuri, bora na zenye bei nafuu.
Licha ya kutazamwa kwa mitazamo tofauti na mataifa mengi yaliyoendelea duniani, Afrika imeonyesha kuwa shughuli nyingi zinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa miaka kadhaa sasa makampuni makubwa kutoka Ulaya, Marekani na Asia yamefungua matawi ya biashara zao na kufanikiwa. Vilevile, maelfu ya biashara mpya zimekuwa zikianzishwa na kufungua fursa nyingi katika sekta mbalimbali.
Afrika ni ya pili kwa kuwa na watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti ukiachana na China, ambapo kwa sasa ina watumiaji wa mtandao wa intaneti takribani milioni 400, ambapo idadi ya Waafrika wote ni zaidi ya bilioni 1.2.
Idadi hiyo kubwa ya Waafrika wanaotumia intaneti imekuja na fursa ya biashara ya mtandaoni ambayo imekuwa ikifanyika kwa miaka takribani 20 sasa katika nchi za Marekani na Ulaya. Aina hii ya biashara inahusisha uuzaji na ununuzi wa bidhaa kutoka kwa wauzaji tofuati kwa njia ya mtandao katika sehemu moja.
Katika mahojiano yaliyofanywa hivi karibuni baina ya mmojawapo wa waanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia, Bw. Sacha Poignonnec na kampuni ya McKinsey & Company ameelezea kuwa mwanzoni ilikuwa ni vigumu kufanya uamuzi wa kufanya biashara Afrika kutokana na changamoto na ugumu ambao waliambiwa wangekutana nao.
“Wakati tunaanza shughuli zetu kwa mara ya kwanza kabisa jijini Lagos nchini Nigeria, tulifungua tovuti yetu hakuna aliyekuwa anatujua lakini wateja walinunua simu za mkononi. Nilishangazwa sana na ile shauku ya wateja kununua bidhaa, tena za gharama ya juu. Cha kustaajabisha zaidi tulifanikiwa kuuza bidhaa na kuzipeleka mpaka walipo wateja. Kwa kweli, ilitia moyo kuona mambo mazuri yakitokea kuliko mabaya tuliyoyasikia,” alielezea Bw. Poignonnec.
“Nina matumaini makubwa na biashara ya mtandaoni Afrika kwasababu kitu cha upekee kuhusiana na bara hili ni kwamba tayari nusu ya idadi ya watu wake wameunganishwa. Kati ya watu zaidi ya bilioni 1.2, milioni 400 wanatumia mtandao wa intaneti. Idadi hii ni ya pili duniani ukiachana na China. Hata hivyo, mbali na idadi hiyo bado kuna mazingira magumu ya usambazaji wa bidhaa na huduma. Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa wateja pale wanapohitaji kufanya manunuzi. Lakini, kwa sababu ya matumizi ya simu za mkononi na intaneti, wateja hivi sasa wanao uwezo wa kuzifikia huduma katika njia iliyo rahisi zaidi,” aliongezea.
Bw. Poignonnec aliendelea mbele zaidi kwa kuelezea kuwa tabia za wateja wanaopatikana Afrika hazitofautiani na sehemu zingine. Mahitaji ni yaleyale. Wanahitaji bidhaa nzuri na bora ambazo zinapatikana kwa bei nafuu. Siku zote wateja wanahitaji kuokoa muda na gharama. Katika maeneo mengi ambayo tunafanya shughuli zetu tunawasaidia wateja kuwa na machaguo mengi ya kununua bidhaa kitu ambacho hakipo katika maeneo wanayoishi.
Katika kipindi cha miaka takribani sita tangu Jumia ianze kufanya shughuli zake barani Afrika changamoto kubwa iliyokumbana nayo ni mfumo wa uendeshaji.
Ameelezea kuwa kwa anayeifahamu Afrika vizuri ni kwamba haina mfumo mzuri wa anwani za makazi katika majiji yake mengi. Hivyo basi kwa watoa huduma kama wao ili kuwafikia wateja vizuri ni lazima washirikiane na wauzaji wa nyumbani ambao ndiyo wanayafahamu vizuri maeneo yao. Kwa mfano, mteja anaweza kuagiza bidhaa lakini anwani ya mahali anapoishi inaweza kuwa ni kwa kuelezea majengo yanayopatikana karibu au shughuli maarufu zinazopatikana eneo alilopo.
Kwa hiyo, endapo ukishirikiana na wauzaji sahihi wanaopatikana kwenye eneo hilo na wenye ufahamu sahihi wa maeneo yao utaweza kuwafikia wateja wote kwa urahisi. Lakini mfumo huu pia nao changamoto zake, vingenevyo uwe na mfumo mzuri wa uendeshaji ambao tumeutengeneza. Tunatumia nyenzo na mifumo ya kiteknolojia ambayo tunawapatia ili waweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, kama vile malipo baada ya bidhaa kufika pamoja na huduma mpaka alipo mteja.
Kuna fursa nyingi endapo waafrika wataamua kuitumia ipasavyo fursa ya biashara kwa njia ya mtandaoni. Tofauti na nchi za Marekani na Ulaya ambapo biashara nyingi huanzia madukani na kuhamia mtandaoni, kwa Afrika wafanyabiashara wengi wanaanzia mtandaoni na kisha hufungua maduka. Sababu kubwa ni kwamba hakuna gharama kufanya biashara mtandaoni.
Ili kujiunga na Jumia kuifanya biashara yako iwepo mtandaoni hauhitaji gharama yoyote kujiunga, hakuna malipo ya kila mwezi au pango la duka, fursa ya kujitangaza na kutafuta masoko ni bure, kuna fursa kubwa ya kuwafikia wateja wengi waliopo maeneo mbalimbali ndani ya muda mfupi pamoja na uhakika wa bidhaa kuwafikia wateja mpaka pale walipo.
Hivyo basi kama mfanyabiashara unaweza ukaanza kidogokidogo mtandaoni, ukawekeza ile faida ndogo unayoipata, baada ya hapo unakua kiasi ambacho unaweza kufungua duka kubwa na kuajiri watu wengi zaidi.

Hivyo makala Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika
yaani makala yote Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mchango-wa-biashara-za-mtandaoni-katika.html
0 Response to "Mchango wa biashara za mtandaoni katika ukuaji wa biashara Afrika"
Post a Comment