Loading...
title : Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli
link : Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli
Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MFANYABASHARA, Henry Munisi (30). Mkazi wa mkoani Mbeya, leo Januari 22, 2019 amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais Magufuli.
Akisoma hati ya Mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Desemba 28, Mwaka Jana huko Jijini Mbeya.
Imedaiwa kuwa, siku ya tukio mshtakiwa Munisi kupitia ukurasa wake wa Facebook alichapisha taarifa za uongo zinazosema "Jinsi Magufuli alivyochota TRIL. 1.5 za ATCL akitumia ujanja wake wa kuleta ndege ili atuibie" huku akijua taarifa hizo ni za uongo na zina lengo la kupotosha umma.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana a baada ya kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho watakaosaini bond ya Sh. Laki tano.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 6. 2019.
Hivyo makala Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli
yaani makala yote Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mfanyabiashara-kizimbani-kwa-tuhuma-za.html
0 Response to "Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli"
Post a Comment