Loading...

MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA

Loading...
MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA
link : MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA

soma pia


MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imewahakikishia wananchi wa Kata ya Wazo kupata maji kuanzia leo usiku.

Akizungumza mbele ya wananchi hao na Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kulikuwa na changamoto kidogo ila kwa sasa wananchi wote waliokuwa kwenye mtandao wa maji wa zamani wataanza kupata maji kuanzia saa 2 usiku.

Luhemeja amesema, mradi huu wa sasa una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita kwa sasa tofauti na ule wa zamani uliokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita elfu sitini na kupelekea mgao wa maji kwenye maeneo mengi.

“Kuanzia sasa hivi hakutakuwa na mgao wa maji kwenye maeneo yote yaliyo na mtandao wa maji, mradi huu una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita na hivyo tatizo la maji kwa Kata ya Wazo, Madale na maeneo mengine limekwisha,”amesema Luhemeja.

Akielezea maeneo ambayo hayajafika mradi kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wa maji, Mhandisi Luhemeja amesema kuna fedha takribani Bilioni 115 zimeshapatikana kwa ajili ya kusambaza mabomba yenye urefu wa Kilometa zaidi ya 1000 katika maeneo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kuna fedha bilioni 115 zimeshatengwa tayari zipo kwenye mchakato wa manunuzi pia tunakaribia kusaini mkataba na mkandarasi ambaye tumeshampata na nitawakaribisha wenyeviti wote kuja kushuhudia ikiwemo na Wakuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,”amesema Luhemeja.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo amesema katika serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli miradi mingi imekuwa ikitekelezwa na wananchi wawe na subira na wameshaahidiwa maji kutoka kuanzia usiku wa leo.

Chongolo amesema, yeye binafsi anaamini kuwa Mtendaji Mkuu wa DAWASA sio mwanasiasa hawezi kudanganya kazi imefanyika na inaonekana ya kutoka uzalishaji wa maji lita elfu sita hadi milioni sita kwa lisaa.

Ameongezea na kusema, atakuja kufuatilia maji kama yanatoka siku ya kesho kutwa (Jumanne) na kujionea kwa machi yake.DAWASA wamedhamiria kufika asilimia 95 Ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kufikia Desemba mwaka huu.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza mbele ya wananchi wa Tegeta Wazo na kuwahakikishia maji safi na salama kufikia leo usiku.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wakati alipotembelea Tenki la maji la Wazo na kuwahakikishia Watapata maji kama walivyoahidiwa na Afisa Mtendaji wa DAWASA
Busta Pampu zilizofungwa kwenye tenki la maji la Wazo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea tenki la maji la Wazo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea mradi wa tenki la maji la Tegeta Wazo lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni sita.


Hivyo makala MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA

yaani makala yote MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mgao-wa-maji-wazo-kuwa-historia-luhemeja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA"

Post a Comment

Loading...