Loading...
title : Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa .
link : Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa .
Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa .
Na HERI SHAABAN
WATUMISHI wa Manispaa ya Ilala watakaotumia vibaya fedha za Serikali kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hayo yalisemwa na Mkugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri wakati wa semina maalum ya force account kwa Watumishi wa Ilala, Maofisa Watendaji Kata, Walimu wakuu wa Msingi , Sekondari na TAKUKURU.
Shauri alisema mafunzo hayo wawezeshaji wametoka Mamlaka za Zabuni za Umma (PPAA)
Alisema dhumuni la mafunzo hayo kuwajengea uwezo Watendaji wa Halmashauri ya Ilala katika matumizi ya fedha za Serikali pindi wanapopewa watumie Kwa dhumuni lililokusudiwa na wale watakaokwenda kinyume wachukulie hatua Kwa mujibu wa sheria za kazi kwa kuisababishia Serikali hasara.
"Kila Mmoja ni kiongozi jukumu lake kusimamia vizuri fedha za Serikali hasa katika miradi ambayo unakabidhiwa nisisikie mtumishi yoyote amekwenda kinyume kwa kutumia madaraka yake vibaya "alisema Shauri.
Shauri alisema Mwaka huu zinatarajia kutumika shilingi bilioni 3 zimeelekezwa katika sekta ya Elimu ambapo kati ya fedha hizo Idara ya elimu msingi milioni 660 na idara elimu sekondari bilioni 2.5 kusudio idara ya sekondari kujenga madarasa 127 .
Mafunzo hayo ya Force account yatawawezesha Kusimamia miradi ya Serikali bila ya kutangaza Wakandarasi au Zabuni .
Alisema watendaji wengi walikuwa hawajui kutumia njia hiyo ya force account wamepewa elimu hiyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumie vizuri fedha ya Serikali.
Katika hatua nyingine manispaa ya Ilala imeunda kamati ya kusimamia ujenzi wa Shule za Halmashauri hiyo.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Serikali kutoka Mamlaka ya Zabuni za Serikali PPAA Hamis Tika alisema Taasisi zote za Serikali zimeshaingizwa katika mfumo huo wa force account ili kuwajengea uwezo watumishi wa Serikali .
Alisema Taasisi za Serikali kama zina wataalam wa kutosha na vifaa wanasimamia mradi kwa gharama nafuu.
Hamis alisema njia hiyo nzuri inapunguza matumizi kwa fedha ndogo za ujenzi na inatumia wakandarasi wake bila watu wa nje.
Alisema mkurugenzi ana uwezo kutumia watendaji wake kusimamia Mradi wowote wa Serikali, sio ujenzi tuu hata Ufundi magari kwa kutengeneza Gari za Watumishi zilizokuwa mbovu.
Hivyo makala Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa .
yaani makala yote Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa . mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mtumishi-wa-ilala-atakayechezea-fedha.html
0 Response to "Mtumishi wa Ilala atakayechezea fedha ya Serikali kutumbuliwa ."
Post a Comment