Loading...
title :
link :
Mwambawahabari
Wananchi wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya kata
Kilio hicho kimetolewa wakati wa kusoma risala ya maendeleo ya kata na msoma risala Felix kapoze alipokuwa akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo kwa muda mrefu jambo linalokwamisha utendaji kazi pamoja na kufanya mawasiliano kuwa magumu.
“Changamoto nyingine kubwa ilipo hapa Kijijini kutokuwapo kwa mtandao wa simu, hii inapelekeana kukwama kwa taarifa nyingi hasa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hivyo tunaiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa itusaidie kupatikana kwa mtandao wa simu ili kurahisisha mawasiliano,” Alifafanua.
Halikadhalika jambo hilo liliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Mh. Desderius Mipata wakati akielezea changamoto hiyo na hatua alizochukua kuhakikisha kuwa mawasiliano hayo yanapatinaka na hatimae kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za maendeleo katika kata hiyo.
“Hawa wananchi ni pekee ambao hawazungumzi na wenzao katika taifa na katika jimbo, juhudi nilizozifanya kama kiongozi wa jimbo ni kuitaka wizara ihakikishe kwamba tunapata mtandao, tunashukuru mungu wametusikiliza na sasa wanajenga minara miwili katika Kijiji cha kilambo cha mkolechi na Kijiji cha Kala, wanasema Kala itazungumza wantuambia katika kipindi kisichozidi miezi miwili,” Alibainisha.
Nae Mh. Wangabo aliwahakikishia wananchi wa kata hiyo kuwa mawasiliano yataimarishwa “Tutaimarisha hayo mawasiliano na juzi nilikuwa naongea na waziri wa ujenzi alikuja pale ofisini na tuliongea swala hili la minara ya mawasiliano, uzuri wameshaanza kufanyia kazi, kwahiyo tutaongeza nguvu kule ili mitandao ya mawasiliano ifanye kazi n ahata radio nkasi iweze kuwafikia huku,” Alisema.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mwambawahabari-wananchi-wa-kata-ya-kala.html
0 Response to " "
Post a Comment