Loading...
title : NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA
link : NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA
NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA
Na Munir Shemweta, WANMM Kigoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewavua nyadhifa zao Wakuu wa Idara za Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya wilaya ya Kigoma pamoja na Afisa Ardhi Mteule kutokana na watendaji hao kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Waliovuliwa nyadhifa zao ni Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Brown Nziku, Emanuel Magembe Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kigoma ambaye pia Afisa Mipango Miji Paul Misuzi.
Mabula alifanya maamuzi hayo jana tarehe 3 Januari 2019 alipofanya ziara ya kushtukiza katika manispaa na halmashauri ya Kigoma wakati akiwa mkoani humo kuhudhuria kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Moyowosi mkoani Kigoma.
Uamuzi wa kuwavua nyadhifa watendaji hao wa sekta ya ardhi unafuatia kushindwa kusimamia maagizo na maelekezo yaliyotolewa tangu mwaka 2017 kuhusu ukusanyaji kodi ya ardhi, uingizaji wamiliki wa viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektronik, utoaji hati kwa wamiliki wa ardhi pamoja na utoaji hati za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi jambo lillosababisha manispaa na halmashauri husika kukosa mapato yanayotokana na kodi ya ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akipata maelezo mara baada ya kuwasili ofisi za halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji alipofanya ziara ya kushtukiza katika manispaa hiyo jana ambapo aliwavua nyadhifa wakuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya wilaya ya Kigoma pamoja na Afisa Ardhi Mteule kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Mwailwa Pangani.
Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Brown Nziku (kulia) na Afisa Ardhi Mteule Paul Misuzi (wa pili kulia) ambao wamevuliwa nyadhifa zao, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kustukiza katika Manispaa ya Kigoma wakati akihudhuria kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Moyowosi Kigoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula akimsikiliza mkazi wa Kigoma Iddy Salum alipowasilisha malalamiko yake kuhusiana na fidia kwenye Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZ) alipofanya ziara ya kushtukiza katika Manispaa ya Kigoma jana wakati akihudhuria kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Moyowosi Kigoma, Katikati ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Magharibi Idrisa Kayera (Picha zote na Hassan Mabuye Wizara ya Ardhi).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/naibu-waziri-mabula-awatumbua-wakuu-wa.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA"
Post a Comment