Loading...
title : NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.
link : NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.
NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimezindua Kozi ya wahudumu wa ndege ili kuhakikisha uwekezaji wa ndege nchini unaendana na Rasilimali watu wenye ujuzi.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kozi hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa kuna mahitaji makubwa katika Sekta ya anga hivyo vyuo viendelee kuzalisha Rasilimali watu ambao wanaweza kutumika ndani na nje ya nchi.
Mhandisi Kamwelwe amesema upatikanaji wa rasilimali watu katika Sekta ya anga ndani changamoto kutokana na kutokuwepo kwa rasilimali hiyo ilisoma katika vyuo vyetu na kuhitajika kwa watu wa nje ya nchi ambao wanalipwa fedha nyingi.
Amesema kuwa uchumi wa viwanda unategemea na usafiri wa anga katika usafirishaji wa bidhaa katika masoko ya nje kwa haraka zaidi.
Kamwelwe amesema kuwa NIT waendelee kubuni zaidi katika kuzalisha Rasilimali watu wa kuweza kuhudumia ndege zetu na kuacha kutegemea rasilimali inayotoka nje ya nchi.
Nae Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa wamejipanga katika uzalishaji wa rasilimali watu katika Sekta ya anga ili kuendana na Uwekezaji wa ndege unaofanywa nchini.Amesema wahudumu ndani ya Ndege ni muhimu sana ambao ndio waangalizi wa usalama wa abiria na mali zao.
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa kozi ya Uhudumu Ndani ya Ndege.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya Uhudumu Ndani ya Ndege.
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo cha Usafirishaji (NIT)
Hivyo makala NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.
yaani makala yote NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/nit-yazindua-kozi-ya-wahudumu-ndani-ya.html
0 Response to "NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege."
Post a Comment