Loading...
title : Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi.
link : Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi.
Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa kutokana na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuimarisha uchumi wake ukusanyaji wa mapato umeimarika.
Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika uwanja wa Gombani Pemba, Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba katika Kilele cha Sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964
Alieleza kuwa jumla ya TZS bilioni 688.7 zilikusanywa mwaka 2017/2018 na Taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) ikilinganishwa na TZS bilioni 521.8 zilizokusanywa na Taasisi hizo mwaka 2016/2017.
Alisisitiza kuwa kiwango hicho ni sawa na ongezeko la TZS bilioni 166.9 sawa na asilimia 32 ambapo mafanikio hayo yameiwezesha Serikali kutekeleza mipango yake ya kuzidi kuinua uchumi na kuwasogezea wananchi huduma za kijamii kwa wepesi na kwa ufansi mkubwa.
Rais Dk. Shein alieleza kuwa kasi ya ukuaji uchumi huo ilikuwa asilimia 7.7 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 5.8 mwaka 2016 ambapo pia, pato la mtu binafisi liliongezeka na kufikia TZS milioni 2.1 sawa na US$ 944 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na TZS milioni 1.89 sawa na US$ 868 mwaka 2016.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa mfumko wa bei nao uliendelea kudhibitiwa katika tarakimu moja katika mwaka 2018 ambapo kasi ya mfumko wa bei ilifikia asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 5.6 katika mwaka 2027.
Hivyo makala Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi.
yaani makala yote Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/rais-dkt-mohamed-shein-aeleza-mafanikio.html
0 Response to "Rais Dkt Mohamed Shein aeleza mafanikio ya Zanzi mikaka 55 ya Mapinduzi."
Post a Comment