Loading...
title : RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo
link : RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo
RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda katika kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika kuhubiri umoja na mshikamano ndani ya Jamii ametangaza kumuenzi kwa kuchagua Barabara moja ya kisasa mkoani humo na kuipa jina la Baba Askofu ili azidi kukumbukwa vizazi na vizazi.
RC Makonda amesema Baba Askofu Pengo amekuwa mfano wa kuigwa katika kuhubiri Amani, Upendo na umoja wa kitaifa na hajawahi kuona haya kukemea uovu wowote jambo ambalo Kama Mkoa umeona ni vizuri kumuenzi kwa kumpatia heshima hiyo.
Kwa upande wake, Baba Askofu Mwadhama Polycarp Kadinari Pengo amemshukuru RC Makonda kwa kutambua mchango wake ambapo amesema ataifanyia maombi barabara hiyo isiwe na matukio ya uhalifu wa ajali.
Hayo yote yamejiri wakati wa ufunguzi wa majengo mapya ya Bweni la wasichana, Ukumbi na gari ya shule ya Sekondari St. Joseph Millennium ya Goba.
Hivyo makala RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo
yaani makala yote RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/rc-dar-es-salaam-kumuenzi-cardinal-pengo.html
0 Response to "RC Dar es salaam, kumuenzi Cardinal Pengo"
Post a Comment