Loading...
title : RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF
link : RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF
RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF
Na John Luhende.
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa ya kujiandikisha kwa lengo la kupata kadi za huduma ya matibabu kupitia Mfuko wa Bima ya Afya NHIF.
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa ya kujiandikisha kwa lengo la kupata kadi za huduma ya matibabu kupitia Mfuko wa Bima ya Afya NHIF.
Amesema wataalamu zaidi ya 1090 watapita katika kila mtaa kwa mana nyumba hadi nyumba ili kuandikisha majina ya wananchi hao ambao wataingia moja kwamoja na kupata huduma hiyo kwa mwaka Mzima.
Makonda aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari ukiwashirikisha wataalamu kutoka mfuko wa Bima ya Afya na mganga mkuu wa Mkoa Grace Maghembe.
Amesema kuwa pamekuwepo na changamoto za kutosha hususani kwenye eneo la afya hivyo kwakutambua hilo Serikali kupitia mfuko wa bima ya afya wamekuja na njia mbadala ya kumaliza tatizo hilo kwakupita kwa wananchi kuandikisha majina.
"Bima hii ni ya Gharama nafuu mno ambapo ukiwa nafamilia ya watu Sita utalazimika kuchangia shilingi 150,000 tu na ukiwa pekee yako utachangia shilingi 40000 hivyo nawaomba wananchi mtoe ushirikiano. "alisema Makonda
Ameongeza kuwa Bima hiyo ya wananchi inawahusu mama ntilie, wanendesha boda boda, pamoja na wananchi wengine wakiwemo akidada wanaouza Bar kwani kuchangamkia huduma hiyo kutapunguza mzigo mzito ambao wanakutana nao wananchi hasa wanapoumwa ghafla.
Makonda pia ametoa pongezi kwa sekta ya Afya ambapo katika mkoa wa Dar es Salaam zimetengwa shilingi bilioni 120 ambazo zinaelekezwa kwenye vituo mbalimbali vya afya kwaajili ya dawa.
"Nitowe rai hata kwenu waandoshi wahabari kujiandikisha katika utaratibu huu kwani na nyie michango imekuwa mingi lakini mkijiandikisha katika kupata huduma hii pia mtapunguza kuchangishana. "alisema Makonda
Kwauopande wake mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Grace Maghembe akizungunza kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa Paul Makonda alisema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa.
Amesema wanaidadi ya wataalamu wasiopungua 1090 ambao watafanya kazi ya kupita nyumba hadi nyumba kuhamasisha na kuandikisha wananchi kwa gharama ya shilingi 25000 kwa kichwa.
Ameongeza kuwa bima hiyo haitakuwa na mipaka katika mkoa wa Dar es Salaam kwamaana kama mtu anaishi temeke anauwezo wakutibiwa ilala na wamefanya hivyo katika kuwaondolea wananchi usumbufu.
Hivyo makala RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF
yaani makala yote RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/rc-makonda-awataka-wananchi-dar.html
0 Response to "RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI DAR KUJIUNGA NA BIMA YA JAMII KUPITIA NHIF"
Post a Comment