Loading...
title : Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani
link : Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani
Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani
Hussein Ndbikile
Mwamba wa habari
Serikali ya Tanzania na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA) zimesaini mkataba wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Gerezani lengo likiwa kupunguza adha ya msongamano jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini humo kabla ya Hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mradi huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Serikali ya Awamu ya Tano wakati ikiomba ridhaa ya kuongoza kwa wananchi na kwamba iliahidi kutekeleza ujenzi wa miundo mbinu imara nchi nzima.
“ Rais John Magufuli anatekeleza ahadi alizowaahidi wananchi, utiaji saini huu inaonyesha wazi Serikali ina mahusiano mazuri na mataifa mengine hata wahisani wana imani na fedha wanazozitoa zinavyotumika,” amesema Waziri Kamwelwe.
Amebainisha kuwa Serikali iko makini katika uboreshaji wa miundo mbinu katika sekta zote ikiwemo usafiri wan chi kavu, angani na majini na kusisitiza ujenzi huo ukikamilika utapunguza adha ya foleni na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Waziri Kamwelwe amesema kuwa bado Serikali inaendelea na ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo ya Ujenzi wa Reli ya umeme( Standard Gauge), viwanja vya ndege, madaraja na barabara.
Kwa uapnde wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Mhandisi Patrick Mfugale amesema mradi huo unatarajiwa kujengwa kwa miezi 24 huku gharama zake zikiwa Sh bilioni 22.48 hadi kukamilika kwake na mkandarasi msaidizi Sh bilioni 2.600.
Mhandisi Mfugale amefafanua kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu mkakati ya kupunguza msongamano huku akibainisha Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction (SMCC) ndio imepewa jukumu la ujenzi.
Katika hatua nyingine, amesema daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 40, upana wa sentimeta 30.4 na njia sita za watembea kwa miguu.
Wakati huo huo, Mhandisi Mfugale amesema Tanroads itahakikisha mkandarasi na mhandisi wanajenga daraja hilo kwa weledi na kukamilisha ndani ya muda.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini, Toshio Nagase amesema utiaji saini mkataba wa mradi huo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Shirika hilo, Shinichi Kitaoka alipotembelea nchini mwaka 2017.
Nagase amesema ana imani mkandarasi aliyekabidhiwa atajenga daraja kwa bora a hali ya juu hata kuliko Daraja la Mfugale.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundo Mbinu, Selemani Kakoso amesema kukamilika kwa daraja hilo kutawasaidia wananchi kuwahi kazini muda wa asubuhi na wakati kurudi nyumbani.
Ameiomba Serikali kutoa fursa kwa wakandarasi wazawa kushiriki kwenye miradi ya ujenzi kwani kuna uthibitisho unaonyesha wakipewa wanafanya kazi kikamilifu akitolea mfano Ujenzi wa Daraja la Mto Mara na Ujenzi wa Meli Ziwa Nyasa na Mwanza.
Hivyo makala Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani
yaani makala yote Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/serikali-ya-tanzania-na-japan-zasaini.html
0 Response to "Serikali ya Tanzania na Japan zasaini Mkataba Mradi wa Ujenzi Daraja la Gerezani"
Post a Comment