Loading...
title : TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO
link : TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO
TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
KATIKA mchakato wa kuendelea kwa michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kuwa itafanya droo ya Kombe hilo siku ya kesho Januari 10 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Hababari katika ofisi za TFF jijini Dr es Salaam. Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo amesema, droo hiyo itakafanyika katika Makao Makuu ya Azam Tv, iliyopo Tabata majira ya saa 5 asubuhi na itahusisha raundi ya 4 zenye timu 32 na raundi ya 5 itakayohusisha timu 16.
Ndimbo amesema timu zilizobaki katika hatua hiyo ni Young Africans SC, Azam FC, Lipuli FC, Mtibwa Sugar, KMC, Coastal Union, Kagera Sugar, Mbeya City, Stand United, JKT Tanzania.
Nyingine ni Singida United, Alliance FC, African Lyon, Biashara United, Boma, Namungo, Mbeya Kwanza, Friends Rangers, Majimaji FC, Dodoma FC, Pamba SC, Rhino Rangers, Reha FC, Dar City, Polisi Tanzania, Mashujaa, Transit Camp, The Mighty Elephant, Cosmopolitan, Kitayosce, La Familia FC, Pan African
Ameongeza, mshindi atakaeibuka katika mashindano hayo ataipeperusha bendera na kuwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, ambapo mwaka jana Mtibwa Sugar ndio waliibuka kidedea wa michuano hiyo.
Hivyo makala TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO
yaani makala yote TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/tff-kutangaza-droo-ya-kombe-la.html
0 Response to "TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO"
Post a Comment