Loading...
title : TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA
link : TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA
TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kampeni za Uchaguzi wa Yanga zimeendelea kwa wagombea kunadi sera zao na kuwataka wanachama kuwapa ridhaa ya kuiongoza Klabu hiyo.Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, leo amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya mwenyekiti katika klabu hiyo
Katika uzinduzi wa kampeni yake, Tiboroha ameweza kuanika vipaumbele vyake iwapo atapatiwa ridhaa na wanachama basi ataanza na mikakati ya muda mfupi ambapo ni kuhakikisha wachezaji wanalipwa mishahara yao kwa wakati na hilo na katika uongozi wake changamoto hiyo haitajitokeza.
Amesema kuwa atahakilisha anajenga na kuimarisha taasisi hiyo kwenye masuala ya Kiuchumi ikiwemo kubadilisha mfumo wa uendeshaji na tayari kuna kampuni mbili zimeshafunguliwa kwa ajili ya uwekezaji zilizo chini ya jina la Yanga
“Tukienda katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji mtu wa kwanza niliyemfikiria ni Mwenyekiti wangu Yusuf Manji kwani ninaamini anaweza kutusaidia kwa sasa nataka aje kuwekeza ili apate faida tofauti na zamani,” amesema Tiboroha
“ Nashangaa kuna watu wanasema mimi nina ugomvi na Manji ila sio kweli nina ushahidi hapa katika simu yangu nimewasiliana nae tena mara kwa mara kwahiyo hayo ni maneno tu yanaongelewa mtaani,” ameongezea.
Pili , Tiboroha amesema atafanya juhudi za haraka kuirudisha klabu kwa wanachama na mashabiki wake. Pia amesema atafanya kazi ya kuimarisha matawi, atajenga mara moja misingi ya uwekezaji na biashara, kuimarisha na kujenga mifumo ya klabu na kushirikisha wadau wote.
Tiboroha amefanya uzinduzi wake makao makuu ya klabu hiyo na kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wanane aliombatana nao, ambao ni Ally Msigwa, Christopher Kashililika, Dominic Francis na Salim Rupia. Wengine ni Arfat Hadji, Said Barala na Peter Simon ambao wote ni wagombea katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Yanga inafanya uchaguzi wa kujaza nafasi Januari 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi ukiwa ni wa kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu katika nyakati tofauti.
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dr Jonas Tiboroha akiwa ananadi sera zake wakati wa uzinduzi wa Kampeni Makao Makuu ya Klabu ya Yanga leo Jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA
yaani makala yote TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/tiboroha-aahidi-kumaliza-tatizo-la.html
0 Response to "TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA"
Post a Comment