Loading...

TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI

Loading...
TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI
link : TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI

soma pia


TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zake iko katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa kuangalia uwekezaji katika Sekta ya Afya katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza  kwenye Kampeni hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Gaudensia Simwanza amesema ziara hiyo katika Hospitali na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya ni kuangalia uwekezaji katika utoaji huduma bora za Afya kwa wananchi,kuhakikisha kuna nguvu kazi imara ya uzalishaji katika Sekta ya viwanda.

Amesema kuwa serikali imewekeza sehemu kubwa ya vifaa na mitambo katika hospitali na hali iliyofanya serikali kuokoa fedha nyingi kutibu wagonjwa nje ya nchi.

Simwanza amesema kuwa Hospitali ya MOI imekuwa na vifaa katika kila idara na kurahisisha utoaji huduma za Afya ambazo ni bora kutokana na Serikali kutilia mkazo uwekezaji wa vifaa tiba,mitambo, Dawa pamoja na vitendanishi.

Nae Afisa Habari wa MOI Patrick Mvungi amesema kuwa MOI itaendelea kutoa huduma bora kutokana na Serikali kuwekeza mashine mbalimbali zilizo kuwa changamoto,ambazo zilikuwa zinasababisha wagonjwa kupewa rufaa.

Mvungi ameipongeza serikali katika uwekezaji uliofanyika Hospitalini hapo pamoja na ujenzi wa majengo ya kisasa na kulaza wagonjwa kwenye 340 vitanda.Amesema katika ununuzi wa vifaa wamenunua Darubin ya kisasa ya sh.bilioni Moja.

Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kissenge amesema serikali imenunua mtambo wa sh.Bilioni Tatu na kufanya Taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma bora za Afya ndani na nje ya nchi.

Kissenge amesema kuwa Taasisi hiyo ni kati ya Taasisi 25 zinazotoa huduma za matibabu ya Moyo katika nchi za Afrika.Amesema magonwa ya Moyo yanatokana na wananchi kushindwa kufanya mazoezi pamoja hali ya ulaji wa vyakula.

Kissenge amesema kuwa nchi ya Thailand wananchi wake wanatumia baiskeli zaidi kuliko magari hali hiyo ni tofauti na hapa nchini ambao wanaona kutembea na magari ni ufahari. 
 Sehemu ya kufanyia  uangalizi wa magonjwa ya mwili wa binadamu kwa kutumia mitambo hiyo ambayo imenunuliwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli katika Hospitali ya MOI. 
 Daktari wa Hospitali ya MOI Ngina Mitti Akizungumza na waandishi wa habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Daktari Bingwa wa Picha za MRI Rahma Hingora akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya katika Hospitali ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam.

 Mgonjwa wa Figo Magesa Masigi akizungumza namna ya huduma za Afya zilizoboreshwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Muuguzi mwandamizi wa Kitengo cha Figo Moroa Nyamatara akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maduka ya MSD Betia Kaema akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
 Duka la MSD lilopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limejngwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
 Afisa Habari wa MOI Patrick Mvungi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Mafanikio ya Miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika uboreshaji wa upatikanaji wa vifaa katika Hospitali hiyo
 Jengo la MOI lilojengwa kwa udhamini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
 Daktari Bingwa wa Hospitali ya MOI Hamis Shaban akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
 Meneja Uhusiano wa NHIF Akizungumza na wagojwa katika Hospitali ya MOI kuhusiana na utumiaji wa bima ya Afya katika Hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
 Jengo la Watoto katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo limejengwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pembe Magufuli.
Moja ya mtambo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI Ulionunuliwa kwa sh.bilioni tatu katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.


Hivyo makala TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI

yaani makala yote TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/timu-ya-maafisa-habari-wizara-ya-afya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI"

Post a Comment

Loading...