Loading...
title : TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA
link : TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA
TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Profesa Adolf Mkenda akizungumza na akizungumza katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha leo. Picha na Vero Ignatus
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa D.Santos Silayo akizungumza katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa TFS Francis Kiondo Mwenyekiti Tughe,Meneja Misitu Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Temeke
Hamisi Jori Afisa misitu wa wakala wa huduma za misitu kanda ya kati Dodoma na mjumbe Baraza
Wakwanza kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Profesa Adolf Mkenda akifuatiwa na Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa D.Santos Silayo. Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) walipokutana Jijini Arusha leo.
Mgeni rasmi pamoja na walio Meza kuu wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa Solidarity Forever.
Mgeni rasmi Profesa Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Na. Vero Ignatus, Arusha
KATIBU Mkuu wa Wizra ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania Tafori na Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo kufanya tafiti maeneo ilioisha miti ili ipandwe mingine kwa ajili ya uvunaji wa haraka utakaoingizia serikali kipato.
Ametoa agizo hilo leo wakati akifungua mkutano wa saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha kukumbushana utawala,haki na wajibu wa Mfanyakazi.
Amesema wajibu mkubwa wa wafanyakazi hao ni kulinda rasilimali za Umma kwa kupambana na uvunaji haramu usiokuwa na utaratibu,uchomaji moto misitu na uvamizi wa mapori kwa ajili ya malisho ya mifugo."Kutokana na hali hii lazima mtafute njia mbadala ya ufugaji wenye tija ili kulinda misitu na mapori yetu na pia kuhakikisha haturuhusu kilimo cha uharibifu wa mazingira,"Alisema Profesa Mkenda
Prof.Mkenda alisema serikali inatambua kazi inayofanywa na wafanyakazi hao na mazingira magumu yanayohatarisha maisha yao,ikiwemo kuzushiwa vitu vya uongo,kupigwa hata kuuwawa, hivyo hawatafungia macho suala hilo.
Ameagiza wafanyakazi hao kuhakikisha wanaacha tabia ya kutoa mizinga bure kwa wafugaji wa nyuki,badala yake wawakodishie ili kuipatia kipato serikali.
"Mizinga hii mnatoa bure lakini wengi hawaitumii,kodisheni ili watu waone uchungu wawese kuitumia ipasavyo kuzalisha asali,"alisema Prof. Mkenda
Alisema Tanzania ina uwezo wa kuongoza dunia kwa uzalishaji asali endapo misiti na mapori iliyopo itatumika vizuri kufunga nyuki ili kujipatia asali ambayo masoko yake yapo.Akitoa mfano alisema mapori ya Kakonko na Kibondo yana misitu na mapori makubwa ambayo tayari serikali imeshapeleka timu ya wataalamu wa kufundisha uzalishaji wa asali kwa wingi ili kukidhi soko la Uholanzi lililopatikana.
Naye Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) D.Santos Silayo, alisema changamoto kubwa walizonazo kwa sasa ni ongezeko la uhalifu maeneo ya misitu,uvamizi,kupambana na ugumu katika kudhibiti wahalifu kwani wengi wao wana silaha za moto.Pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni misiti mingi ipo nje ta maeno yaliohifadhiwa rasmi,watumishi kutishiwa na kuzuiwa kutekeleza majukumu yao na baadhi ya watumishi wasiozingatia kanuni na sheria za uwajibikaji kazini.
"Kutokana na hali hiyo TFS inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu za kudhibiti hali hiyo kwa watakaobainika,"alisema Pofesa Silayo.Pia amesema TFS wanatarajia kuanzisha mfuko wa kuweka akiba na kukopa SACCOS, kwa wafanyakazi wao na kujali afya za wafanyakazi wao wawapo kazini.
Hivyo makala TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA
yaani makala yote TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/tuna-kazi-kubwa-ya-kupanda-miti-nchi.html
0 Response to "TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA"
Post a Comment