Loading...
title : WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO
link : WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO
WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO
WANAFUNZI wote 272 wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Tabata Dar es Salaam, waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamefaulu kwenda kidato cha tano huku 204 kati yao wakipata daraja la kwanza na la pili.
Kwa mujibu wamatokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wanafunzi 86 wa shule hiyo wamepata daraja la kwanza na 118 daraja la pili.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa wanafunzi wengine 60 wamepata daraja la tatu na wanafuni nane daraja la nne lakini wote wamefanikiwa kupata alama za kuendelea na kidato cha tano.
Mkuu wa Taaluma shuleni hapo, John Kishefu alisema matokeo hayo ni mazuri sana hasa ikizingatiwa idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa nao ambayo ni kubwa kuliko shule nyingi zilizofanya mtihani huo.
Kishefu alisema miaka yote Tusiime huwa haichagui wanafunzi wa vipaji maalum kama zinavyofanyaa baadhi ya shule bali huchukua wa aina zote hata wale wenye uwezo mkubwa na mdogo darasani na kuwaandaa vizuri.
“Sisi hatuchagui mwanafunzi, unaweza kukuta amekuja hapa akiwa na uwezo mdogo sana lakini timu mahiri ya walimu waliopo hapa wanamtengeneza hadi anapata daraja la kwanza au la pili hilo nji jambo la kawaida hapa Tusiime,” alisema Kishefu
Kishefu alisema matokeo hayo mazuri ni mwendelezo ya matokeo kama hayo kwa shule za Tusiime kuanzia shule ya msingi na kidato cha pili ambapo wamekuwa wakifaulisha kwa alama za juu.
“Matokeo haya yamewafurahisha hata wazazi wengi ambao wamekuwa wakitupigia simu na kutupongeza. Tulikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi lakini tumemudu kuwapeleka kidato cha tano wote hii si kazi rahisi,” alisema Kishefu
“Wanafunzi wetu wengi wamepata alama A za kutosha sana kwenye masomo mbalimbali na siku ya leo (jana) simu zetu zilikuwa busy wazazi wanapiga kuelezea namna walivyofurahishwa na matokeo haya,” alisema Kishefu
Akizungumzia matokeo hayo, Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, alisema matokeo hayo mazuri yanatokana na dhamira waliyonayo kama taasisi kuhakikisha vijana wa Tanzania wanapata elimu bora katika mazingira yaliyo safi na salama.
“Napenda kuwathibitishia wadau wote wa elimu kuwa shule za Tusiime zimejipanga kuendelea kutoa elimu bora hapa nchini na hivyo tumewekeza vya kutosha katika miundombinu, zana za kufundishia, motisha kwa wafanyakazi na ushirikiano mzuri baina yetu, serikali na wazazi, haya yote kwa pamoja ndiyo yametufikisha kwenye matokeo haya,” alisema
Alisema shule hizo zimejipanga kuendelea kufanya vizuri kwa kuimarisha mifumo ya utoaji wa elimu na huduma katika shule hizo ili kuwajengea watoto uwezo na kuwapa maarifa stahiki na aliwataka wazazi waendelee kuwaamini na kuwapa ushirikiano katika azma yao hiyo ya kutoa elimu bora kwa vijana.
Hivyo makala WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO
yaani makala yote WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/wanafunzi-wote-tusiime-waliofanya.html
0 Response to "WANAFUNZI WOTE TUSIIME WALIOFANYA MTIHANI KIDATO CHA NNE MWAKA JANA WAFAULU MTIHANI ,KUENDELEA KIDATO CHA TANO"
Post a Comment