Loading...

Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu

Loading...
Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu
link : Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu

soma pia


Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewaagiza wasanii walioingia mikataba na kampuni za simu au mawakala kwa ajili ya kutumia kazi zao kama miito ya simu lakini hawajalipwa stahiki zao, wawasilishe katika ofisi hizo kwa ajili ya kupatiwa haki zao kuanzia 2016 hadi 2018

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, ameyasema hayo kumaliza kikao na wasanii na mawakala waliokuwa wakijadili kuhusu kutokuwapo na mgawanyo sawa wa malipo ya miito ya simu baina ya wasanii wa muziki, kampuni za simu na mawakala wanaouza kazi za wasanii na kufanya wasanii hao kupoteza haki zao.

Katika kikao hicho, walikubaliana malipo kuwa kwa kipindi cha miezi sita ya kutafuta suluhu ya kudumu, malipo ya kazi za wasanii, mawakala, kampuni za simu na mtoa huduma yawe 50 kwa 50 kabla ya kuja na mfumo rasmi.

“TCRA tumekutana na wadau wote ili kupata muafaka na hatimaye pasiwepo na malalamiko tena kutoka upande wowote na tukakubaliana kuwa kampuni za simu ziwasiliane na wasanii moja kwa moja badala ya kuishia kwa mawakala,” amesema.

Amesema wamekubaliana kuwa upo uwezekano wa msanii kusaini makubaliano ya kutumiwa kwa kazi zake kama miito ya simu kwenye kampuni husika ya simu moja kwa moja na endapo atataka kutumia wakala afanye hivyo.

Pia walikubaliana kuwa kampuni za simu ziwasilishe TCRA mgawanyo halisi wa gharama za utayarishaji wa kazi hizo za wasanii ambazo hutumika kama miito ya simu.

Mhandisi Kilaba, amesema azimio lingine ni TCRA kuangalia uhalisia wa mikataba inayoingiwa baina ya kampuni za simu na mawakala au wasanii kuona kama ni rafiki katika mazingira ya biashara ya miito ya simu kuangalia unufaika kwa wasanii.

Kilaba amesema June mwaka huu, tutakuwa tumeshaangalia namna ya gharama watakazokuwa wanalipana kati ya kampuni za simu, mawakala na wasanii.

Aidha amesema mwaka jana walikuwa na kikao kwa ajili ya kujadili wanafanya nini na walikutana na mitandao yote ya simu. Lengo kufahamu nini kinaendelea katika kazi za wasanii wanazozitumia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi mwafaka waliyofikia katika mapato yatokanayo na miito ya simu kwa miziki ya wasanii.
 Wadau wa muziki wa wakijadili mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.
 Msanii Abdul Nasibu (Diamond Platinum) akichangia Mada ya mapato yatokanayo na miito ya simu katika mkutano ulioitishwa na TCRA.
 Mkutano kati ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)   na Wadau wa muziki wakiwa katika mkutano wa kujadili kufikia mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.
Wadau wa muziki wakijadili mwafaka wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na miito ya simu.


Hivyo makala Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu

yaani makala yote Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/wasanii-waagizwa-kuwasilisha-mkataba-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wasanii waagizwa kuwasilisha Mkataba na kampuni za simu"

Post a Comment

Loading...