Loading...
title : WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA
link : WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA
WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji sehemu ya matofali aliyotoa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi wapata fursa ya kusoma
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akilakiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe Jijini Tanga wakati alipokwenda kuwakabidhi matofali na mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akikagua madarasa kwenye ambayo hayajakwisha kwenye shule ya Sekondari Pongwe kabla ya kuwakabidhi mifuko ya saruji na matofali kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM) Mbaraka Sadi akizungumza kulia ni MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu |
sehemu ya mifuko ya saruji ilioyotolewa na Waziri Ummy |
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe wakifuatilia hotuba ya MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya Sekondari Pongwe
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katikati ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mikanjuni mara baada ya kukabidhi msaada wa matofali na mifuko ya saruji
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye hafla hiyo
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Tanga na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo amekabidhi matofali 3,500 zenye thamani ya shilingi milioni 5.6 na mifuko ya Saruji 250 yenye thamani ya shilingi milioni 3 ili kuweza kusaidia kutatua tatizo la uhaba wa madarasa.
Msaada huo aliuta kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya Sekondari zilizopo katika Jiji la Tanga ambazo ni Shule za Sekondari Pongwe, Maweni, Mikanjuni, Horten na Kiomoni ambapo kila shule imepatiwa Matofali 700 na saruji mifuko 50.
Akizungumza ktk makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mikanjuni, Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM)alieleza kufurahishwa na jitihada za Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli za kuboresha Elimu nchini na katika Jiji la Tanga
Alisema juhudi hizo zimesaidia kuwezesha uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na Elimu ya Sekondari katika Jiji la Tanga. Hivyo yeye kama mbunge ameona anao wajibu wa kuchangia ujenzi wa madarasa ili kuwezesha watoto wote 6,024 wa Jijini Tanga waliofaulu Elimu ya Msingi kuendelea na Elimu ya Sekondari.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Tobias Mwilapwa alisema katika mwaka huu 2019 jumla ya wanafunzi 6,024 wamefaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza katika Jiji la Tanga kutoka wanafunzi 5,332 mwaka 2018.
Hali hii imesababisha mahitaji zaidi ya Vyumba vya madarasa 71 ili kumudu kuchukua ongezeko la wanafunzi 1,324 waliofaulu kwenda Sekondari katika Jiji la Tanga.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga Ndugu Kidima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Bwana Daudi Mayeji, Waheshimiwa Madiwani wa Kata husika, Watendaji wa Idara ya Elimu na Bodi za Shule husika.
Hivyo makala WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA
yaani makala yote WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/waziri-ummy-achangia-vifaa-vya-ujenzi.html
0 Response to "WAZIRI UMMY ACHANGIA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA"
Post a Comment