Loading...
title : Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria
link : Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria
Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria
Waangalizi wa uchaguzi wanakosoa kuchelewesha ufunguaji wa vituo katika maeneo mengi nchini Nigeria, wakisema uchelewashaji huo na kuahirishwa kwa uchaguzi huo kwa wiki nzima viliwakatisha tamaa watu wengi kupiga kura.
Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika umesema katika ripoti yake kuwa uchaguzi ulipita kwa amani kwa sehemu kubwa licha ya matukio kadhaa wa kadhaa ya vurugu na udanganyifu.
Kundi la Situation Room, ambalo ni muungano wa mashirika ya kiraia yaliosimamia uchaguzi huo kw apamoja, limesema watu wasiopungua 39 waliuawa nchini Nigeria kote kwenye siku ya uchaguzi.
Kundi la waangalizi wa Jumuiya ya Madola limezitaja vurugu zilizoukumba uchaguzi huo kuwa suala linalohuzunisha na mwenyekit wake, rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema Nigeria ingeweza kufanya vizuri zaidi.
"Kumekuwa na ugumu wa kimandalizi, kilojistiki na kiufundi katika uchaguzi huu ambavyo tunajua na kuamini kuwa INEC na wadau wote nchini Nigeria watahitaji kuvishughulikia.
Jambo la pili, vurugu zinazohusiana na uchaguzi na upotevu wa maisha vilivyotokea katika maeneo kadhaa vinasikitisha. Naamini Nigeria inaweza kufanya vizuri zaidi. Vurugu hazina nafasi katika demokrasia ya kisasa."
Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya Maria Arena amesema kura hiyo ilitatizwa na kosoro za kiutendaji zilizosababisha ugumu kwa wapigakura.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osibanjo.
Hivyo makala Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria
yaani makala yote Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/buhari-apata-ushindi-wa-kwanza-nigeria.html
0 Response to "Buhari apata ushindi wa kwanza Nigeria"
Post a Comment