Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa. - Hallo rafiki
SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts
makala afya,
makala general,
makala kisiasa,
makala kitamaduni,
makala kiuchumi,
makala mambo mapya,
makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.
title :
Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.link :
Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.
Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.
 |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Timo Soini (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. Dkt. Mahiga yupo nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Waziri Mahiga na ujumbe wake (kushoto) ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland na ujumbe wake.
 |
Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Timo Soini.amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji.
Pongezi hizo alizitoa wakati alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambaye yupo nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 25 na 26 Februari 2019.
Kwenye mazungumzo yao, Mawaziri hao wamesisitiza umuhimu wa Tanzania na Finland kuboresha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za biashara, uwekezaji, mafunzo ya ufundi, ajira kupitia sekta ya misitu, ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa kwa kuzingatia usawa, pamoja na kuwajengea uwezo wanawake na watoto.
Aidha, Mhe. Soini alitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na mchango mkubwa katika usuluhishi wa migogoro inayozikabili baadhi ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Hivyo, walikubaliana kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, na matishio ya ugaidi.
Kabla ya mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Sampo Suihko, Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha OMNIA Espoo ambaye alieleza utayari wa Taasisi yake wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kubadilishana uzoefu wa kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi yanayoendana na soko la ajira.
Mhe. Mahiga pia alifanya mazungumzo na Mhe. Matti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Finland na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro. Mhe. Ahtisaari aliipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya katika utatuzi wa migogoro kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu na kusihi kuendeleza jitihada hizo kwa ustawi wa Dunia nzima.
Vilevile, Dkt. Mahiga alifanya mazungumzo na Bw. Jukka Kallio, Makamu wa Rais wa Helsinki. Katika mazungumzo hayo, uongozi wa Bandari ya Vuosaari umeahidi kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha mifumo ya kidigitali (Digitalization) itakayoongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
Katika kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini, Mhe. Waziri Mahiga alifanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara (Business Finland) na Makampuni makubwa ya kibiashara nchini humo. Wafanyabiasha hao walipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na waliahidi kuwekeza na kushawishi makampuni mengine kuona umuhimu wa kuwekeza nchini Tanzania.
Mhe. Waziri anahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Bi. Anne-Mari Virolainen, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland; Bw. Mauri Pekkarinen, Naibu Spika wa Bunge la Finland, Bw. Juhan Damski, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya nchini Finland na baadaye kuzungumza na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Finland.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
26 Februari 2019 |
|
Hivyo makala Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.
yaani makala yote Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/finland-yaipongeza-tanzania-vita-dhidi.html
Related Posts :
Nishati : Dk. Mwinuka Awapongeza Wahandisi Wanawake TANESCO
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwaki… Read More...
Elimu : UKAID na Wizara ya Fedha na Mipango yazindua Programu ya Mafunzo kwa Watumishi
Wafanyakazi watano wa Wizara ya Fedha na Mipango (Walioketi) waliopatiwa udhamini wa masomo nchini katika vyuo vikuu nchini Uingereza k… Read More...
DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Waha… Read More...
Matukio : Mbunge Ritta Kabati Apokea Kero za Wenyeviti wa Mitaa ,Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya… Read More...
Mazingira : Mbunge Mussa na Mkewe Washiriki zoezi la Msaragambo wa Mtaro, Maweni Tanga
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akichukua sururu kwa ajiliu ya kushiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya M… Read More...
0 Response to "Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa."
Post a Comment