Loading...
title : GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU
link : GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU
GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU
*Watayarishaji wa filamu waaswa kutengeneza filamu zenye ubora viwango
*Lengo la tamasha ni kukuza tasnia ya filamu na sio kujinufaisha kama taasisi
Na.Khadija seif,Globu ya jamii
TAMASHA la filamu la kimataifa la sinema(SZIFF) limetangaza filamu zilizopita katika mchujo wa mwanzo (nomination) ili kuwania tuzo za sinema zetu kwa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar,Mkurugenzi wa uendeshaji wa Azam Yahya Mohammed amesema tuzo za filamu za kimataifa za sinema zetu(SZIFF) zimegawanyika katika makundi mawili , swahili panorama na sinema za kimataifa( WORLD CINEMA) .
Mohammed amefafanua zaidi katika mchakato huo tuzo nne zimeingia katika kipengele cha tamthilia bora,Mwongozaji bora,mwandishi bora na mhariri bora wa picha jongevu, ambapo tamasha hilo linatarajiwa kufanyika febuari 23 mwaka huu.
"Jumla ya tuzo 30 zitatolewa kwa washindi ambapo washindi watapata zawadi ya kati milioni moja hadi milioni tano kulingana na ukubwa wa tuzo,lakini pia washindi watapata cheti pamoja na tuzo,"alisema Mohammed.
Aidha Mwenyekiti wa jopo la Majaji Martin Mhando amesema upatikanaji wa washiriki katika kila kipengele ulizingatia vigezo vingi na filamu zilizoshinda katika duru la pili ni zenye ubora wa hali ya juu.
"Mchakato wa kuonyesha filamu ulianza rasmi mwanzoni mwa mwezi januari lengo lilikuwa ni kuwaongezea ujuzi waandaji,watayarishaji pamoja na wasanii katika kuboresha kazi za", alisema Mhando.
Wasanii walioingia kwenye duru hilo la pili ni kwa upande wa kiume na wanashindania kipengele cha Msanii bora wa kiume ni pamoja na gabo,hemed, hassan kazoa pamoja na salum mkopi huku filamu zao pia zikiingia kwenye duru hilo huku msanii bora wa kike akishindanishwa Monalisa ,wema sepetu na wengine.
Ametoa wito kwa wadau wa tasnia ya filamu kutengeneza filamu zenye ubora ambazo zitaweza kufikia soko la kimataifa na kutambulisha utamaduni wa kitanzania kupitia mavazi,lugha pamoja na nyimbo zinazotumiwa kwenye filamu hizo.
Kwa upande wa Mratibu wa tamasha hilo Sophia Mgaza amesema kwa mwaka huu kumekuwa na mafanikio makubwa baada ya filamu nyingi kutoka mikoani kuingia katika duru la pili tofauti na msimu uliopita.
"Mchakato wa mwaka huu amekuwa wa kipekee kutokana na uhai ndani kuongezeka ,huu inaonyesha ishara kwanza tasnia ya filamu unazidi kuongezeka na kukua na ubora wa kazi za filamu umekuwa mkubwa tofauti na ilivyokuwa mwaka Jana ," alisema Mgaza.
Pia ameeleza filamu zilizotangwa Leo kuingia katika mchujo wa pili ni zile zilizokidhi vigezo ambazo zimegawanyika katika makundi mawili ,kundi la filamu zote ndefu,f upi na pamoja na zilizopigiwa kura na watazamaji kwa njia ya simu huku kundi la mwisho likiwa limepitishwa na jopo la majaji.
"Ni matarajio yetu kuwa tamasha litasaidia kukuza taaluma ya filamu na kuongeza ubunifu na kutambua vipaji na ufanisi uliopo katika tasnia pamoja kuongeza hamasa kwa watengenezaji na watazamaji wa filamu za kiswahili ," alisema Mgaza.
Mratibu wa Tamasha la sinema zetu (SZIFF) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitambulisha filamu 30 zilizoingia kwenye duru la pili jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Azam Yahya Mohammed akitolea ufafanuzi mchakato wa upatikanaji wa filamu 30 bora zilizotinga fainali leo jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa jopo la majaji Martin Mhando akitolea ufafanuzi vipengele vilivo shindanishwa katika tamasha la sinema zetu( SZIFF ) jijini Dar es salaam
Hivyo makala GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU
yaani makala yote GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/gabo-angara-duru-ya-pili-tamasha-la.html
0 Response to "GABO AN'GARA DURU YA PILI TAMASHA LA SINEMA ZETU"
Post a Comment