Loading...
title : IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA
link : IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA
IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA

Mgeni rasmi wa uzinduzi wa Usajili wa vyeti vya Ndoa na safari za Ibada ya Hijja Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wa pili kutoka kushoto, kaimu sheikhe wa Mkoa huo alhaji sheikhe Hasan Kabeke wakiomba dua iliyoongozwa na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Ali Hamis Ngeruko (kulia) baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuzindua mkakati huo juzi
………………….
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
IBADA ya Hijja nchini Saudi Arabia imeibua fursa za kibiashara kwa Watanzania hivyo wanatakiwa kuchangamkia ili wanufaike kiuchumi.
Hayo yalielezwa juzi jijini Mwanza na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Ali Hamis Ngeruko wakati wa uzinduzi wa elimu ya Hijja na Usajili wa Vyeti vya Ndoa kwa waumini wa dini ya kiislamu uliofanyika kitaifa jijini humu.
Alisema Ibada hiyo ya Hijja ni jambo linalohitaji elimu kwa kuwa giza haliwezi kuongoza jambo, hivyo ufinyu wa elimu husababisha watu wengi kuharibu mengi ukiwemo uhusiano wao kwa ujinga na wengine huendelea kuharibu.
Alieleza kuwa soko hilo lililopo Mina huko Makka kuna fursa ya soko la kimataifa la mifugo, vyakula, mikeka na tasbihia lakini bado Watanzania hawajalitambua wala kufikiria kutumia fursa hizo kibiashara zilizopo kwenye mji huo Mtakatifu wakati wa Ibada ya Hijja na kunufaika kiuchumi.
“BAKWATA Taifa imeona izindue elimu ya Ibada ya Hijja Mwanza na kila mkoa utafanya kazi hiyo , utasimamia na kuelimisha waumini.Pia Uhusiano na ushirikiano wa Serikali na BAKWATA upo kwenye mambo mbalimbali japo baadhi ya watu wanaweza kuona uzinduzi wa elimu ya Hijja una uhusiano gani au hauna uhusiano,” alisema.
Nguruko alieleza zaidi kuwa Tanzania imejaaliwa madini na vito yanayotumika kutegeneza tasbihi, wana mifugo na nguo (vitenge) hivyo Watanzania wakiitumia fursa hiyo wataingiza fedha nyingi za kigeni kutokana na kuuza bidhaa za aina hiyo Makka lakini wamelalia soko hilo.
“Watanzania tutanufaika na mengi kwani Makka si ibada tu, kuna biashara inafanyika pia na kwa kuwa tunayo mikeka, vitenge, madini na mifugo na mchele bado soko hilo hatujaliona na haliwezi kutambuliwa bila kutambulishwa.Hivyo watu wawe na maarifa na hijja yao pamoja na neema watumie fursa zilizopo Makka,”alisema mjumbe huyo wa baraza la Ulamaa.
Kwa mujibu wa Nguruko waumini wanaokwenda kuhiji wanatakiwa kuchangamkia fursa za soko la Makka ambalo raia wengi wa nchi za Afrika Magharibi (Nigeria, Cameroon na Senegal) ndio pekee wamelitumia kwa uchumi wa nchi zao na mtu mmoja mmoja kunufanika nalo kwa kupeleka na kuuza bidhaa zao huko.
Kwamba tasbihi , mikufu, mikeka na vitenge ni ubunifu wa watu wa mataifa hayo ambao umewanaingizia vipato vizuri kupitia Makka huku biashara ya mifugo na mchele ikifanywa na raia wa kutoka Thailand na Australia na kuhoji “ sidhani kama Watanzania tunalitambua soko hilo , tumelala na mifugo yetu na mchele.”a
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye mgeni rasmi alisema hakuwahi kufikiria fursa za kiuchumi kwenye Hijja hivyo Watanzania wazione, wajue watanufaika nazo vipi iwe kwa Waislamu na wasio Waislamu.
Alisema jambo hilo serikali italibeba na BAKWATA taifa kwa upande wao walichukue na kuwataka waumini wa dini ya kiislamu waliowekeza nchini waone watakavyoshiriki kwenye fursa hizo ingawa kinachoangaliwa zaidi ni ubora wa bidhaa na mifugo.
Mongela alipongeza utaratibu huo unaofanywa ndani ya BAKWATA kuwa ni mapinduzi na migogoro iliyokuwepo wakati Hijja itakwisha na kuifanya serikali itapate ahuweni kwa kuwa nchi yetu haina dini ila wananchi wake wana dini.
Naye kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasan Kabeke alisema BAKWATA kutoa elimu hiyo ya safari ya Ibada ya Hijja inalenga kuwazindua Waislamu ikiwa ni pamoja na kutumiza majukumu yake kwa mujibu wa katiba ya baraza hilo.
Alifafanua kuwa Tanzania imetengewa nafasi za mahujaji 23,000 lakini wanaojaaliwa kwenda ni 2,500 hadi 3,000 kulinganisha na Kenya inayopeleka mahujaji 4,500 hivyo Waislamu wanayo fursa bado ya kwenda kuhiji kwa gharama ya sh. 10,105,000 sawa na Dola 4300 za Marekani
Hivyo makala IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA
yaani makala yote IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/ibada-ya-hijja-yaibua-fursa-za.html
0 Response to "IBADA YA HIJJA YAIBUA FURSA ZA KIBIASHARA"
Post a Comment