Loading...

ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI

Loading...
ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI
link : ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI

soma pia


ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI

Serikali imetoa kiasi cha shilingi 5,558,604,325.95 kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa Wilaya ya Hai kuanzia Desemba 2015 ambapo kati ya fedha hizo shilingi 1,633,980,574.16zimetumika kugharamia elimu bila malipo kwa shule za msingi na 3,924,623,751.79 kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Hali hiyo imesababisha ongezeko la uandikishaji wanafunzi ngazi ya awali kutoka 3,843 mwaka 2015 hadi kufikia 4,127 mwaka 2018 na msingi kutoka 4,201 mwaka 2015hadi kufikia 4,758 mwaka 2018.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitatu katika wilaya ya Hai, Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya amesema sera ya elimu bila malipo kwa watoto wenye umri kwenda shule imefanya watoto wengi kutoka kwenye familia duni kupata fursa hiyo muhimu kwa ajili ya maendelo ya taifa.

Alisema serikali imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ufuatiliaji wa shule ambapo kwa mwaka 2018 Wilaya ilikabidhiwa pikipiki 17 kwa ajili wa waratibu elimu kata ikiwa ni sambamba na uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba 35madarasa ya elimu msingi, matundu 120 ya vyoo.

Aliongeza kuwa Wilaya imepokea walimu 22 wa masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya walimu kutoka 118 hadi walimu 140 katika juhudi za kuimarisha masomo ya sayansi shuleni.

“Kutokana na juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu pamoja na usimamizi na ufuatiliaji unaofanywa na viongozi wa ngazi zote, Wilaya ya Hai ilishika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya nane kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana” Alisisitiza Sabaya.

Mbali na elimu; Sabaya alisema pia serikali imeendela kutoa fedha kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) katika mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo hadi Desemba 2018 jumla ya shilingi 3,049,467,299.98 zimetolewa kwa kaya 3,890 walizotumia kuanzisha miradi midogomidogo inayowapatia kipato ikiwemo kufuga kuku, kilimo cha bustani za mbogamboga na biashara mbalimbali.

Akizungumzia sekta ya Afya; Dc Sabaya alisema kiasi cha shilingi 1,496,355,495.00 zimetumika kununua dawa na kufanya kiwango cha upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 90.57 ukilinganisha na asilimia 73.59 ya mwaka 2014.

“Tunaendelea kuboresha sekta hii muhimu na tumejenga duka la dawa linalotoa huduma kwa gharama nafuu saa 24 kwa wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali nadni na nje ya wilaya” alisema.

“Tumekamilisha wodi ya wanawake katika hospitali ya wilaya, kukamilika kwa miundo mbinu hii muhimu kumewapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma na kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanalazimika kwenda Hospitali ya Mkoa Mawenzi’alisisitiza Sabaya.

Katika kuboresha sekta ya umwagiliaji; serikali kwa kipindi hicho imetoa shilingi 844,000,000 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa mifereji 3 ya umwagiliaji ili kuongeza eneo la umwagiliaji kwa lengo la kuimarisha uzalishaji.

Aidha wilaya ya Hai imeanzisha kilimo cha mazao mawili ya biashara ambayo ni Korosho na vanilla kwa lengo la kuinua uchumi wa mkulima.

Akizungumia huduma ya maji Sabaya alisema serikali imetoa kiasi cha shilingi 4,062,951,699.35 kuimarisha usambazaji wa maji ambazo zimetumika kufanya ujenzi na upanuzi wa mradi wa maji wa Losaa-Kia, kujenga vituo 58 vya kutolea huduma kwenye vijiji 10 vya Mkalama, Mijongweni, Ngosero, Mbatakero, Mungushi, Kimashuku, Sanya Station, Tindigani, Mtakuja na Chemka.

Naye mgeni wa heshima Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndugu Kheri James alipongeza ushirikiano ulipo kati ya viongozi wa Wilaya ya Hai na kutaka hali hiyo iendelezwe.
Kheri alisema kuwa juhudi zilizoonyeshwa na waatalamu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya na Kamati ya ulinzi na usalama imeifanya Wilaya kuwa ya kwanza Kimkoa na ya kumi kitaifa katika ukusanyaji wa mapato na kwamba hali hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,  Ndugu Kheri James  akinyoosha juu ngao aliyokabidhiwa na wananchi wa Wilaya ya Hai kumpelekea Mhe. RAis wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya .

 Aliyekuwa mhandisi wa Ujenzi, Msangi akibadhiwa zawadi kutokana na usimamizi bora ya miradi ya ujenzi

 Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni wa heshma kutokana na usimamizi na ufuatiliaji bora uliofanya wilaya kushika nafasi ya kumi kitaifa.
  Viongozi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,  Ndugu Kheri James  (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Kumotola Kumotola; Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Godwin Mollel; Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya  na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai Mhe. Wang’uba Maganda.



Hivyo makala ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI

yaani makala yote ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/ilani-ya-ccm-inavyotekelezwa-wilaya-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ILANI YA CCM INAVYOTEKELEZWA WILAYA YA HAI"

Post a Comment

Loading...