Loading...

KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI.

Loading...
KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI.
link : KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI.

soma pia


KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, wakiwa katika kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies wakati walipofanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akimkabidhi Kitabu chenye Fursa na Miradi yenye Uhitaji Mitaji ya Uwekezaji nchini , Mwekezaji toka nchini Uturuki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MNG Group of Companies mara baada ya kufanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.


Wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies wakifuatilia kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (hayupo pichani), wakati walipofanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini, tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akiongea na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies, wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiwasikiliza wataalamu wa masuala ya uwekezaji wa Ofisi ya waziri Mkuu wakati wa kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies (hawapo pichani), wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.


Na. OWM, DODOMA.

Kampuni ya MNG Group of Companies ya nchini Uturuki imeonesha nia ya kufanya uwekezaji mkubwa nchini katika sekta mbalimbali; zikiwemo sekta za Uchukuzi, Utalii, Nishati na Usafiri wa Anga.

Uwekezaji huo umebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya MNG Group of Companies, Mehmet Gunal, wakati alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki (Mb), jijini Dodoma, tarehe 5 Januari 2019.

Waziri Kairuki amebainisha kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha uwekezaji wenye tija nchini, na kwa kutumia mfumo wa sera ya Ushirikiano baina ya sekta Binafsi na Umma inahakikisha inavutia wawekezaji zaidi nchini.

“Tunazo fursa na miradi inayohitaji mitaji ya uwekezaji hapa nchini, jukumu letu ni kuhakikisha wawekezaji mnapata mazingira wezeshi katika fursa na miradi mnayotaka kuwekeza ili nchi iweze kupata tija kutokana uwekezaji huo” Amesisitiza Mhe. Kairuki.

Akiongea katika kikao hicho mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MNG Group of Companies, Mehmet Gunal, amefafanua kuwa , Kampuni hiyo iko tayari kuwekeza nchini katika Sekta mbalimbali, kwa kuwa wamevutiwa na mazingira ya uwekezaji ya hapa nchini.

Aidha, Gunal alifafanua kuwa wamejipanga kutumia fursa na miradi yenye kuhitaji uwekezaji nchini ili kuweza kufanya uwekezaji mkubwa , pia alisema kampuni yake ipo tayari kuwekeza hata kwa mfumo wa sera ya ushirikiano baina ya Sekta ya Binafsi na Umma au kuwekeza wao wenyewe.

Kampuni ya MNG Group of Companies inao uzoefu katika masuala ya uwekezaji kwa miaka 42 katika mabara matatu Duniani, ikiwa imejikita katika uwekezaji kwenye sekta sita na tayari hadi hivi sasa imetekeleza miradi zaidi ya mia mbili katika mabara hayo.

Baadhi ya Miradi ambayo imetekelezwa na Kampuni hiyo ni pamoja na , Bwawa la kufua Umeme la Chief Dam la nchini Algeria, Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa KOTOKA (terminal III), wa nchini Ghana, Ujenzi wa makao makuu ya na Benki ya Halk nchini Uturuki.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, Wataalamu wa masuala ya Uwekezaji na maendeleo ya Sekta Binafsi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini.


Hivyo makala KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI.

yaani makala yote KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/kampuni-ya-uturuki-yaonesha-nia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAMPUNI YA UTURUKI YAONESHA NIA KUWEKEZA SEKTA ZA UCHUKUZI, UTALII, NISHATI, USAFIRI WA ANGA NA UJENZI."

Post a Comment

Loading...