Loading...
title : KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA
link : KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA
KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA
Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka nchini imetangaza kulipekeka tamasha hilo kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa Sumbawanga,mkoani Rukwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam , Msama amesema wakazi wa Sumbawanga wamekuwa wakihitaji huduma ya tamasha hilo kwa muda mrefu, hivyo ameahidi kuikata kiu ya wakazi wa mji huo kwa namna ya kipekee kabisa.
“Sumbawanga wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusu kutokupelekewa Tamasha hilo, Mwaka huu kwa Mara ya kwanza tutapeleka Tamasha kwa wakazi wa Sumbawanga, wakae tayari kupokea ujio wa Tamasha lililobeba utofauti” amesema Msama.
Amesema katika Tamasha la mwaka huu kutakuwa na utofauti mkubwa, ambapo ameeleza kuwa wapo waimbaji wapya ambao hawajawahi kuja nchini, na kuongeza kuwa kwa Mwaka huu waimbaji wote watakaopata nafasi watalazimika kuimba kwa kutumia Band (LIVE) na si CD (PlayBack) kama ilivyozoeleka.
“Tumeongeza Waimbaji wapya ambao hawajawahi kuja nchini, waimbaji ambao hawataweza kuimba live kwakweli watatusamehee bure,itakuwa vigumu kupokea ushiriki wao kwenye tamasha hilo,tunafanya yote hiyo kuhakikisha tamasha la Pasaka 2019 linakuwa lenye utofauti mkubwa ,n ahata wapenzi wa muziki huo waone utofauti mkubwa na si vinginevyo”aliongeza Msama.
Akizungumzia kauli ya tamasha hilo,Msama ametaja kuwa ni “ Umoja na Mshikamano hudumisha amani ya nchi yetu” alisema na kuongeza kuwa ni lazima Watanzania tukubali Mungu ametupa Rais mzuri na mchapa kazi,tutamuombea kokote tutakaposimama na ninawaomba Watanzania kwa ujumla wetu tumuombee Rais wetu.
Tamasha hilo la Pasaka linatarajiwa kufanyika April, 21, 2019 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama ambapo ameahidi Tamasha hilo kuwa lenye utofauti Mkubwa ukilinganisha na Matamasha yote yaliyopita.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka Alex Msama akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari leo Ofisini kwake,Kinondoni jijini Dar wakati akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka,ikiwemo kutangaza kulipeleka tamasha hilo kwa mara ya kwanza mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo Ofisini kwake,Kinondoni jijini Dar kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka 2019,ikiwemo kutangaza kulipeleka tamasha hilo kwa mara ya kwanza mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa.
Mmoja wa Waandishi wa habari kutoka ZBC akiuliza swali kwa Mwandaaji wa tamasha la Pasaka,Alex Msama.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo kuhusu maandalizi mbalimbali ya tamasha la Pasaka
Hivyo makala KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA
yaani makala yote KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/kwa-mara-ya-kwanza-tamasha-la-pasaka.html
0 Response to "KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA"
Post a Comment