Loading...
title : LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA
link : LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA
LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA
Na Felix Mwagara, MOHA-Arumeru
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku na kutoa onyo kali kwa magari ya polisi nchini kutumika kubeba au kusindikiza dawa za kulenya.
Lugola amesema wapo baadhi ya polisi wanatuhumiwa kufanya matukio ya kubeba bangi, mirungi pamoja na dawa aina mbalimbali za kulenya hapa nchini wakitumia magari ya Jeshi la Polisi ambapo ni kinyume cha sheria.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Mkoani Arusha, jana, mara baada ya kukabidhiwa gari la polisi lililokarabitiwa na Kampuni ya Friedkin Conservation Fund (CFC) ya hapa nchini kwa gharama ya shilingi milioni 15, amesema kitendo hicho kinalifedhehesha Jeshi la Polisi ambalo linatakiwa kuwa mfano wa kukabiliana na uhalifu.
Kutokana na tabia mbaya hiyo walionayo baadhi ya polisi nchini wasiokua waadilifu, Waziri Lugola amesema polisi yeyote akikamatwa kushiriki kufanya tukio hilo hata muonea huruma kamwe, ataondolewa katika nafasi hiyo na kushtakiwa.
“Polisi wakikamatwa wanasindikiza au kubeba dawa za kulevya, polisi hao tutawafukuza kazi pamoja na kuwashtaki, gari hili la polisi ambalo limekarabatiwa na Taasisi hii, litumike vizuri kwa kupambana na wahalifu na siyo vinginevyo,” alisema Lugola.
Aidha, Mbunge wa Viti Maalum wa CCM Wilayani humo, Amina Mollel alimlalamikia Waziri Lugola akisema ndani ya Wilaya hiyo kuna kesi ambazo zinachukua mda mrefu katika vituo vya polisi kwa kisingizio cha upelelezi kuwa haujakamilika hasa kesi za ubakaji ambapo alitoa namba ya faili mkutanoni hapo.
“Mheshimiwa Waziri, licha ya kuwa Polisi wanafanya kazi vizuri wilayani hapa Arumeru lakini kuna tatizo la kesi mbalimbali zinachukua muda mrefu katika vituo vya polisi hasa kesi za kubaka, na kuwafanya wananchi kuchelewa kupata haki zao, kesi inachukua miezi sita bado ipo katika upepelezi, huo muda ni mrefu sana” alisema Amina.
Hata hivyo, Waziri Lugola kutokana na tuhuma hiyo, alimuagiza Mkuu wa Polisi wilayani humo (OCD) kutafuta faili la kesi zilizotajwa na Mbunge huyo ili aweze kumletea katika mkutano huo kabla ya kumaliza mkutano huo.
Baada ya kutoa agizo hilo, OCD alileta faili hilo katika mkutano huo, na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya hiyo, ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Jerry Murro, ili aweze kumkabidhi Waziri Lugola na aweze kutoa maelekezo zaidi.
Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo anatembelea Wilaya zote za Mkoa huo akifuatilia utendaji kazi wa Taasisi zake ambazo zipo ndani ya Wizara yake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Soko la Ngaramtoni, Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, leo, akitoa onyo kwa baadhi ya Polisi nchini wenye tabia ya kubeba, kusindikiza dawa za kulevya kwa kutumia magari ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka Arusha, Amina Mollel.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akipokea ufunguo wa gari la Polisi namba PT 0747, kutoka kwa Kampuni ya Friedkin Conservation Fund (FCF), Mratibu wa Shughuli za Kudhibiti Ujangili, William Mallya (kulia) ambayo ilikarabati gari hilo la Kituo cha Polisi Usa-River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Lugola mara baada ya kulikabidhi gari hilo kwa Jeshi la Polisi wilayani humo, alitaka gari hilo litumike vizuri kubebea watuhumiwa na sio kubeba au kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jerry Muro
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akilikagua gari la Polisi namba PT 0747 ambalo limekarabatiwa na Kampuni ya Friedkin Conservation Fund kwa ajili ya Kituo cha Polisi Usa-River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Lugola alikabidhiwa gari hilo na pia naye akalikabidhi kwa Jeshi la Polisi Wilaya hiyo na kuagiza litumike vizuri kubebea watuhumiwa na sio kubeba au kusindikiza dawa za kulevya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto, akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro (katikati), wakati Waziri huyo alipokuwa anaelekea kupokea madarasa yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule ya Msingi Usa-River, Wilayani humo, Mkoa wa Arusha. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, James Mchembe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hivyo makala LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA
yaani makala yote LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/lugola-atoa-onyo-magari-ya-polisi.html
0 Response to "LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA"
Post a Comment