Loading...
title : MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI
link : MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI
MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI
Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari wakiwa tayari kuzungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor akizungumza na wanafunzi leo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma
Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kilakala akizungumza. Lydia Churi Ntambi
Na Lydia Churi-Mahakama, Dodoma
Mahakama ya Tanzania imeanzisha mpango wa kushirikiana na vyuo na shule za sekondari katika kuwalea na kuwatambua wanafunzi wenye vipawa, tabia na maadili mema ambapo huwafuatilia na kuwafanyia tathmini ili baadaye waje kufanya kazi na Mahakama pamoja na maeneo mengine katika sekta ya Sheria
Katika wiki ya utoaji wa elimu ya Sheria inayoendele jijini Dodoma, wanafunzi kutoka baadhi ya vyuo vikuu na shule za sekondari nchini wanashiriki kwa kujifunza masuala ya mbambali yanayohusu sheria pamoja na taratibu za kimahakama jijini.
Akizungumza na Wanafunzi, Waalimu na Washauri wa wanafunzi hao, kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Latifa Mansoor amesema kupitia Mpango huo wa Mahakama, watumishi watakaoajiriwa na Mahakama ni wale tu wenye tabia na maadili mema na wenye uwezo uliothibitika ili waweze kutoa huduma bora hapo baadaye.
Akizungumzia utekelezaji wa mpango huo, Jaji Mansoor amesema baadhi ya mambo ambayo Mahakama inashirikiana na vyuo na shule hizo ni kuwa na mahusiano ya karibu na kuwa na fomu za ufuatiliaji wa mienendo ya maadili na taaluma za wanafunzi ambazo hujazwa na kutumwa kwa Mahakama ya Tanzania mara mbili kwa mwaka.
Aliyataja mambo mengine ya ushirikiano kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa klabu na utoaji wa elimu ya sheria mashuleni pamoja na mpango wa kuwazawadia fursa za masomo na zawadi nyingine wanafunzi wenye vipaji na maadili mema.
Aidha, Jaji Mansoor pia aliwataka Waalimu na washauri wa shule hizo kuwalea na kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanakuwa na ubora katika taaluma, tabia na maadili. Aliongeza kuwa wanafunzi wa vyuo hufuatiliwa na kumbulkumbu zao huhifadhiwa kwa mahitaji ya baadaye ikiwemo ajira kwa watumishi wa Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.
Aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa na tabia na maadili mema kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.” Tunawaalika katika maadhimisho haya ili kubadilishana uzoefu na pia mjifunze masuala mbalimbali ya sheria ili muwe na ufahamu zaidi”, alisema.
Kufuatia Mpango huu wa ushirikiano, Mahakama ya Tanzania inatarajia kuwa na huduma zilizoimarika, watumishi kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu na kwa kuzingatia utawala wa sheria, na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili kupungua.
Vyuo ambavyo mpaka sasa vimeingia kwenye ushirikiano na Mahakama ya Tanzania ni vyuo vikuu vya Dar es salaam, Mzumbe, Dodoma, Ruaha, Iringa na chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Shule za sekondari ni pamoja na Maua Seminari. Kisimiri, Shule ya Wavulana Ilboru, Shule ya sekondari Kilakala, Shule za Sekondari za Wavulana za Feza, Marian na Tabora. Nyingine ni Shule ya sekondari Msalato na Mazinde Juu.

Hivyo makala MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI
yaani makala yote MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mahakama-yaanzisha-mpango-wa-kuwalea.html
0 Response to "MAHAKAMA YAANZISHA MPANGO WA KUWALEA WANAFUNZI KIMAADILI"
Post a Comment