Loading...

MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE

Loading...
MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE
link : MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE

soma pia


MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad ametekeleza ahadi ya kuchangia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule zilizopo katika kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Azza amekabidhi mabati hayo yenye futi 10,Februari 16,2019 kwa viongozi wa vijiji vya Masunula na Usule ikiwa ni ahadi aliyotoa Oktoba 15,2018, alipotembelea kata ya Usule na kuelezwa kuwa shule hizo zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Akizungumza wakati wa zoezi kukabidhi mabati lililoshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko, Azza alisema mchango wake huo ni sehemu ya kuboresha shule ya Masunula ambayo kwa miaka mitatu mfululizo (2016,2017 na 2018) imekuwa ikiongoza kwa shule za serikali mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya darasa la saba. 

“Nilipewa malalamiko ya vyoo shule ya msingi Usule na shule ya msingi Masunula,nikaahidi kuchangia mabati 20,leo nimekuja kukamilisha ahadi yangu,hivyo nakabidhi mabati 10 yenye futi 10 kwa kila shule”,alisema. 

Mheshimiwa Azza aliwataka wananchi kuacha kufanya siasa kwenye masuala ya maendeleo huku akiwahamasisha wananchi kujenga vyoo kwenye nyumba zao. Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala alimshukuru mbunge huyo kutekeleza ahadi yake na kuongeza kuwa tayari matundu 14 ya vyoo yamejengwa katika shule ya Masunula na sasa wanaendelea na shughuli ya kuezeka majengo ya vyoo hivyo. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kusomesha watoto wao na kuachana na tamaa za kuwaozesha huku akiwataka kutumia fedha wanazopata kutokana na kilimo kujenga nyumba za kisasa. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Masunula, Kiyenze Majinge (CUF). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Usule na Masunula.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala akimshukuru mbunge Azza Hilal kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika eneo ambapo pamejengwa vyoo vya shule katika shule ya msingi Masunula. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akieleza jambo katika eneo la ujenzi wa vyoo kwenye shule ya msingi Masunula. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Hivyo makala MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE

yaani makala yote MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mbunge-azza-hilal-atekeleza-ahadi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE"

Post a Comment

Loading...