Loading...

Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar

Loading...
Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar
link : Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar

soma pia


Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar

Na ANDREW CHALE, ZANZIBAR

KUNDI la wanamuziki wanaokuzwa la Mkubwa na Wanawe usiku wa 7 Februari 2019 limeweza kukonga nyoyo za watu waliojitokeza kushuhudia tamasha la 16 la Kimataifa la Sauti za Busara, kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja.

Kundi hilo limeweza kuonesha umahri wao wa kuimba na kucheza jukwaani huku wakiendana sambamba na mapigo na ala za muziki wa bendi ‘live' iliamsha shangwe za mara kwa mara kwa mashabiki waliofurika Ngome Kongwe.

Vijana hao wa waliweza kuimba nyimbo zaidi ya tano (5) ikiwemo ya Stata ukiimbwa na mwanadada Catrima Wegesa huku nyimbo zingine zikiimbwa na Abdala Mustapha 'Kisamaki' huku kijana mdogo kabisa wa kundi hilo Abdul Kadry 'Dogo Kadry' akiwa kivutio kila alipopanda kuimba kwenye jukwaa hilo la Busara.

Dogo Kadry aliweza kuimba nyimbo zaidi ya mbili ikiwemo ule aliyourudua wimbo wa Asu ulioimbwa na Abdul Misambano. pia waliweza kuimba nyimbo za wasanii waliowahi kupitia kundi hilo zikiwemo za ‘Mototo wa udongo’ na ‘Watakubali'. Kundi hilo lililo chini ya muasisi wake, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule ya wilayani Temeke, Dar es Salaam hadi sasa lina vijana wanaofanya kazi za Sanaa za Muziki zaidi ya 100.

Miongoni wa wasanii waliowahi kuwa kwenye kundi hilo na kwa sasa wanajitegemea ni pamoja na Dogo Aslay, Mboso na wengine wengineo.Miaka miaka kadhaa iliyopita wasanii hao Dogo Aslay na Mboso waliwahi kushiriki tamasha hilo huku wakiwa vijana wenye umri mdogo ambapo walikuwa kivutio kama ilivyo kwa sasa kwa msanii mpya wa kundi hilo Dogo Kadry ambaye kwenye shoo hiyo aliweza kuonesha uwezo wake licha ya kuwa na umri wa chini ya miaka 15.

Mpaka sasa Mkubwa na Wanawake Crew wameshatoa nyimbo mbalimbali zikiwemo : Tofauti, 2012; Nawashusha Down, 2013; Fanya Yako, 2014; Unanitusi, 2015; Sitakitararira, 2016; Naelewa, 2016; Yerere, 2016Lakini pia baadae waliweza kutoa nyimbo kupitia bendi ya Yamoto ambapo napo walitoa nyimbo mbalimbali .
 Kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwaa katika onesho lao la jana usiku 7 Februari 2019, kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar
Mmoja wa Wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe, Abdala Mustapha 'Kisamaki' akionesha uwezo wa kuimba na kucheza jukwaani wakati wa tamasha hilo la Sauti za Busara, 7 Februari 2019
 Msanii mwenye umri mdogo katika kundi hilo la Mkubwa na Wanawe, Abdul Kadry 'Dogo Kadry' akiimba kwa hisia nyimbo ya Asu.
 Dogo Kadri akifanya mahojiano baada ya kumalizika kwa  shoo yao hiyo
shangwe zilizokuwa zikiendelea wakati wa shoo hiyo


Hivyo makala Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar

yaani makala yote Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mkubwa-na-wanawe-wakonga-nyoyo-sauti-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkubwa na Wanawe wakonga nyoyo Sauti za Busara Zanzibar"

Post a Comment

Loading...