Loading...

MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

Loading...
MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU
link : MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

soma pia


MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji ( TBC) Dkt. Ayub Rioba akibadilishana mawazo na Mawakili wa Serikali Obadia Kajungu na Anna Mkongwa wakati alipotembelea Banda la Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Mkurugenzi Mkuu amesifu uhusiano na ushirikiano mzuri wa kikazi kati ya TBC na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.



Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Dr. Ayoub Rioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Utangazaji ( TBC), amesifu na kupongeza ushirikiano mzuri anaoupata kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Amesema, uhusiano wa kikazi kati ya Taasisi hizi mbili, umekuwa na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Chombo hicho cha Taifa cha Habari na kwamba, ni matumaini yake uhusiano huo utaendelea kwa maslahi na maendeleo ya Taifa. 

Ameyasema hayo siku ya Jumanne, wakati alipotembelea Banda la maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘ Square’, Jijini Dodoma 

“ Hongereni sana kwa maonesho haya. Mimi niwashukuru sana kwa ushirikiano na mahusiano mazuri ambayo tunayo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hasa katika eneo la mikataba. Sisi kama Chombo cha Habari cha Serikali tunaitegemea sana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa ushauri wa kisheria na upitiaji wa mikataba yetu ya kibiashara” akasema Mkurugenzi Rioba 

Na kuongeza “ Kwa mazingira ya kazi zetu, na hasa pale tunapohitaji kununua vifaa au mitambo ya radio au televisheni ni lazima tulete mikataba yetu kwenu ili iweze kupatiwa ushauri wa kisheria. Kwa hiyo upitiaji wa mikataba yetu na kutolewa kwa wakati ni jambo lenye tija kwetu na katika utekelezaji wa majukumu yetu kwa maneno mengine sisi ni wadau wenu”. 

Akatoa mfano kwa kusema pala kifaa kinapo haribika labda kwa kupigwa na radi ni wazi kwamba mchakato wa kukinunua ukiwamo mkataba lazima ufanyike na uhusishe Ofisi yenu, na uharaka wa ununuzi wa kifaa hicho na kwa kuwa radio au televisheni haiwezi kutokuwapo hewani kwa muda mrefu ndiyo maana kutoka na unyeti huo hata mchakato wake unabidi uwe wa haraka lakini kwa kuzingatia matakwa ya kisheria. 

Mawakili wa Serikali, Obadia Kajungu na Anna Mkongwa waliokuwa wakitoa huduma za ushauri kwa wageni waliokuwa wakifika katika Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, walimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TBC kwa kufika katika banda hilo. 

“Tunakushukuru kwamba unaridhishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo baina yetu. Ushauri ulioutoa hasa wa upitiaji wa mikataba na kuitoa kwa wakati tutauzingatia na kuufisha ngazi za juu. Tukushukuru pia kwa kututembelea katika banda letu na kujielimisha kuhusu majukumu na utendaji kazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu” akasema Wakili Obadia Kajungu. 

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwa ni Mdau wa Mahakama ilishiriki maonesho hayo yaliyoanza Januari 31 na kukamilika Februari Tano. Huduma zilizotolewa na Mawakili wa Serikali kwa wageni waliofika kwa shinda mbalimba ni pamoja na, kutoa ushauri wa kisheria, kujibu na kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto za kisheria ambazo baadhi ya wageni walikuwa nazo, kuelezea na kufafanua nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ujumla. 

Baadhi ya wageni walielekezwa wapi au Taasisi gani wanapashwa kwenda kupata msaada ziadi wa shida zao. Pia Mawakili wa Serikali hao walitoa huduma ya uelimishaji kwa wanafunzi wa sekondari na Vyuo Vikuu waliofika au kupangiwa katika banda la Mwanasheria Mkuu ikiwa ni sehemu ya mfunzo . 


Hivyo makala MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

yaani makala yote MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mkurugenzi-mkuu-tbc-asifu-uhusiano-wake.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU"

Post a Comment

Loading...