Loading...
title : MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA
link : MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA
MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA
Kwa niaba ya familia nzima ya Benki ya CRDB nitoe pole kwa familia nzima ya Clouds Media Group, familia ya Prof. Mutahaba, Tasnia nzima ya Habari na Burudani na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na rafiki, ndugu na kaka yetu kipenzi Ruge Mutahaba. Amahakika Taifa limepoteza mtu mahiri sana katika tasnia ya habari na burudani.
Pamoja na majonzi makubwa tuliyonayo, sisi Wanafamilia wa Benki ya CRDB, tunajivunia sana ndugu yetu Ruge Mutahaba. Ruge pamoja na Joseph Kusaga ndio waasisi wa uhusiano huu mkubwa tunaouona leo hii baina ya Benki yetu ya CRDB na Clouds Media. Tukiwa Benki ya Kizalendo azma yetu kubwa nikuona tunaishi ndoto za Watanzania walio wengi.
Wakati Ruge na Kusaga wanakuja na wazo kuanzisha redio, ili kuwa ni ndoto, lakini uthubutu wao wa kufuata fursa ndio ulioishawishi Benki yetu kuwaamini na kuwapa mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 40 uliofanikisha kuanzishwa kwa Clouds FM redio. Sasa hivi Clouds FM inazaidi ya miaka 19, pamoja na kuanzishwa kwa media nyengine Choice FM, Clouds TV, Clouds International, Clouds Digital pamoja na kuvuka mipaka na kuingia Rwanda, Botswana na Abudhabi.
Hizi zote ni jitihada na maono ya ndugu yetu Ruge Mtahaba, hakuna asiyefahamu bidii na umahiri wake katika kazi na ndio maana sisi Wanafamilia ya CRDB tutaendelea kumshukuru Mungu kwa ajili yake, tumejifunza mengi kutoka kwakwe na tunamshukuru kwa kutupa nafasi ya kuishi ndoto hii ya Clouds Media Group ambayo leo hii imewafungulia dunia Watanzania wengi hususani vijana.
Katika sifa kuu aliyokuwa nayo ndugu yetu Ruge Mutahaba kubwa zaidi alipenda sana maendeleo ya watu wengine, nadhani hii inajidhihirisha kupitia program yake fursa. Siku zote alikuwa akitambua umuhimu wa kuielimisha jamii katika masuala mbalimbali. Amekuwa na mchango mkubwa sana katika kutusaidia kufikisha elimu juu ya huduma zetu za kifedha kupitia Clouds Media, tumekuwa tukishirikiana kwa karibu sana.
Utayari wetu wa kushirikiana na Clouds Media katika nyanja mbalimbali ni kwasababu siku zote tumekuwa tukijuwa msimamo wake katika kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguuka. Maisha yake yamekuwa ni baraka kwa wengine na daima tutaendelea kumuenzi. Mioyo yetu imejawa na huzuni, lakini daima tutakwenda kusherekea maisha ya ndugu yetu Ruge Mutahaba.
Inna lilah wa inna ilayh raji’un
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza nawaandishi wa habari alipofika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba, kuhani msiba. Mikocheni jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajidi Nsekela akiwa na baadhi ya waombolezaji wengine waliofika kwenye msiba wa Ruge Mutahaba, Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
Hivyo makala MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA
yaani makala yote MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mkurugenzi-mtendaji-wa-benki-ya-crdb_28.html
0 Response to "MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA"
Post a Comment