Loading...
title : MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA
link : MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA
MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MTANZANIA Nabbed Abdul Rahman Asman (42) amekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bali nchini Indonesia baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Methamphetamine ambazo alizimeza na kukutwa ndani ya tumbo lake.
Jarida la Citizen limeeleza kuwa mamlaka ya usalama nchini Indonesia imeeleza hayo mapema jumanne, na hiyo ni baada ya mamlaka ya uhamiaji kitengo cha kuzuia dawa za kulevya kueleza kuwa walimkatama Nabbed Abdul Rahman Asman akiwa na dawa hizo uwanjani hapo mapema Januari 30 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa zaidi ya kilo moja za Methamphetamine zilizokuwa zimemezwa na Asman ziligundulika kupitia mashine za x-Ray na Ct scan, Mamlaka hiyo imeeleza kuwa takriban vifuko 99 vilivyowekwa unga mweupe vilifika zaidi ya kilo moja.
Asman (42) anashikiliwa na vyombo vya dola nchini humo na bado haijafahamika kama atahukumiwa kifo na hiyo ni baada ya nchi hiyo (Indonesia) kuwa moja ya nchi ambazo zina msimamo na sheria kali dhidi ya dawa ya kulevya diniani.
Matukio mengine ya kukamatwa madawa ya kulevya nchini humo ni pamoja na lile la Husein Ashad Bhari (60) kukamatwa na kilogram 45 za Marijuana na akahukumiwa miaka 15 jela, na wengine kadhaa waliokamatwa na dawa hizo kuhukumiwa kifo.
Hivyo makala MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA
yaani makala yote MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mtanzania-ashikwa-na-kilo-za-dawa-za.html
0 Response to "MTANZANIA ASHIKWA NA KILO ZA DAWA ZA KULEVYA ALIZOMEZA NCHINI INDONESIA"
Post a Comment