Loading...

NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

Loading...
NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
link : NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

soma pia


NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI




 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na viongozi wa Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo (Kulia) ni Afisa Ustawi wa Jamii, Bi. Felisiana Mboya

 Mwamba wa habari
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ameviasa Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kuendeleza ustawi wa Watu wenye Ulemavu.
Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo alipofanya ziara Mkoani Dodoma kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ndani ya mkoa huo, ambapo alikutana na viongozi Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu.
Mhe. Ikupa alieleza kuwa ushirikiano baina ya Serikali na vyama vya watu wenye ulemavu ni muhimu katika kuhakisha haki na masilahi ya watu wenye ulemavu yanalidwa kwa kuzingatia Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali.
“Serikali imeendelea kuchukua hatua na kutekeleza jukumu lake la kuhamasisha na kuwalinda watu wenye ulemavu nchini kwa kuhakikisha haki za kundi hilo maalumu zinatekelezwa,” alisema Ikupa
Aidha, alisisitiza uongozi wa Mkoa kuhakikisha unahusisha mahitaji maalumu ya wenye ulemavu katika bajeti wanazozitenga, kutoa elimu na taarifa juu ya upatikanaji wa dawa, mafuta ya watu wenye ualbino na vifaa saidizi, na uundwaji wa kamati za kuhudumia wenye ulemavu.
Aliongezea kuwa, ni vyema Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na maafisa ustawi wa jamii wakahakikisha wanawasaidia watu wenye ulemavu wanapokabiliana na changamoto kwenye uandikaji wa maandiko ya kuomba mikopo.
“Unakuta kikundi cha watu wenye ulemavu wanakuwa wabunifu na wanawazo zuri la kuanzisha mradi au biashara lakini wanakumbana na changamoto ya kuaandaa andiko la miradi yao na hivyo kuwafanya wakate tamaa mapema,” alisema Ikupa
Pia, aliwasii Maafisa Ustawi wa Jamii kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu wenye ulemavu na kuendelea kuweka mifumo mizuri ya kutunza taarifa hizo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Bw. Edward Mpogolo aliunga mkono na kuyapokea maelekezo yote ya Naibu Waziri na kumhakikishia kuwa Mkoa wa Dodoma utakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza maagizo aliyoyatoa.
 “Tutafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Vyama vya Watu wenye Ulemavu ili kuangalia namna bora ya kuwahudumia kwa kuzingatia mahitaji yao,” alisema Mpogolo.
Naye Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Bw. Justus Ng’wantalima alimpongeza Naibu Waziri kwa jitihada ambazo amekuwa akizifanya katika kutetea Watu wenye Ulemavu.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Ikupa, alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Chama cha Walemavu Sulungai kinachojishughulisha na ushonaji wa viatu vya wazi (kobasi) na utengenezaji wa majiko. Vilevile Mhe. Ikupa alitembelea shule ya Viziwi iliyopo Jijini Dodoma.


Hivyo makala NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/naibu-waziri-ikupa-ahimiza-vyama-vya_13.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI"

Post a Comment

Loading...