Loading...
title : NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA
link : NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA
NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akizungumza na wanachama wa Sulungai, alipokuwa kwenye ziara kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma. (Kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo.
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Sulungai (CHAWASU) Bw. Stanley Jumbe akimweleza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa namna ya kuandaa viatu vya wazi aina ya Makobazi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akitengeneza viatu vya wazi (Makobazi) alipotembelea Chama cha Walemavu Salungai kilichopo Kata ya Ipagala, Jijini Dodoma. (Kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akinunua viatu vya wazi aina ya Makobazi kwa Chama cha Walemavu Sulungai (CHAWASU) alipotembeleaa Kikundi hicho kilichopo Kata ya Ipagala kujionea shughuli zinazofanywa na wajasiriamali hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na Chama cha Walemavu Sulungai (CHAWASU), Viongozi na Watendaji wa Jiji la Dodoma alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akieleza jambo wanafunzi wa shule viziwi iliyopo Jijini Dodoma(hawapo pichani), alipotembelea shule hiyo kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Mwananfunzi mwenye Uziwi wa darasa la Tatu, Shadia Kizamo akitaja jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri y Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kwa lugha ya alama swali aliloulizwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Mwananfunzi mwenye Uziwi wa darasa la Saba, Eliabi Chilongola akimweleza kwa lugha ya alama Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, teknolojia aliyoivumbua ya Umwagiliaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akimsikiliza Mratibu wa Shule maalumu ya Viziwi Dodoma, Bw. Robin Donilergoed (wa pili kutoka kulia) alipokuwa akikagua miundombinu ya Shule hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wenye Uziwi wanaojishughulisha na ufundi wa Ushonaji.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Hivyo makala NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/naibu-waziri-ikupa-atembelea-kukundi.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA"
Post a Comment