Loading...

RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA

Loading...
RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA
link : RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA

soma pia


RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.

Waziri Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa

Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.

Pia, Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.

"Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 27, 2019.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA

yaani makala yote RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/ruge-alikuwa-mstari-wa-mbele-kuwasaidia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...