Loading...

SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO

Loading...
SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO
link : SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO

soma pia


SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO

Na WAMJW – DSM

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amewaasa Wazazi na Walezi nchini kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata huduma za chanjo ili kujikinga dhidi ya maradhi yanayozuilika kwa chanjo.

Waziri Ummy amesema haya leo wakati akipokea majokofu ya kutunzia chanjo na vishikwambi (Tablets) kwa ajili ya kukusanya taarifa za chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.

Waziri Ummy alisema kuwa imethibitika kuwa yapo magonjwa zaidi ya 20 nambayo yanadhibitika kwa njia ya chanjo hivyo ni muhimu kwa wazazi na walezi ambao hawajawapeleka watoto kupata chanjo kuitumia fursa hii ili watoto wao wapate chanjo

“Sasa hivi imeshathibitika kuna magonjwa zaidi ya 20 ambayo yanadhibitika kupitia njia ya chanjo , ni lazima wahakikishe Wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao kupata chanjo , ni lazima wapate tena dozi zote.” Alisema Waziri Ummy.

Waziri ummy, alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na shirika la gavi, imefanikiwa kununua jumla ya majokofu 1,385 yenye thamani ya shilingi bilioni 13,991,270,300, huku ikichangia kwa 20% na gavi 80%, kwa ajili ya kuimarisha mnyororo baridi wa utunzaji wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.

Aliendelea kusema kuwa Majokofu 1,190 yanatumia nishati ya jua na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 10,879,000 na majokofu 195 yanatumia umeme, na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 5,361,000.

Vilevile Waziri ummy alisema, Serikali na shirika la Gavi imenunua jumla ya vishikwambi (tablets) 1,249 vyenye gharama ya shilingi  bilioni 1,598,720,000 kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi taarifa za chanjo kwa njia ya mtandao, na kila kishikwambi kina thamani ya shilingi milioni 1,280,000.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa mapema mwezi Mei tutapokea jumla ya vishikwambi 2100 venye thamani ya shilingi bilioni 2,688,000,000 na mwishoni mwa mwaka huu, tutapokea awamu nyingine ya majokofu yenye thamani ya shilingi bilioni 11,533,357,820 na kufikia asilimia zaidi 80 ya mahitaji ya majokofu na vishikwambi katika vituo vyote hapa nchini.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa Halmashauri zote za Tanzania Bara pamoja na Wilaya za Zanzibar zitapokea majokofu haya kwa awamu kuu mbili, ambapo Awamu ya kwanza itahusisha mikoa 15 ambayo ni Dodoma, Geita, Kagera, Kigoma, Lindi, Tanga, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Songwe, Unguja, Pwani na Singida huku awamu ya pili itahusisha mikoa iliyobaki.

Hata hivyo, katika kuhakikisha ufanisi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa majokofu ya kuhifadhia chanjo, Wizara ya Afya kwa kushikiana na wadau wa shirika la JSI na Nexleaf kwa ufadhili wa Gavi, inatarajia kufunga vifaa vya kupima na kufuatilia halijoto katika vituo takribani 5,000 kati ya vituo zaidi ya 7,000 kote nchini.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, Vifaa hivi vinamuwezesha Afisa Chanjo kujua utendaji kazi wa jokofu ikiwa ni pamoja na kujua halijoto ya jokofu katika vituo vya huduma za afya bila ya kulazimika kufika katika kituo husika, Vifaa hivi vinatuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pindi halijoto inapopanda au kushuka.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kulia)  akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari wakati akipokea majokofu ya kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung  (kulia) akieleza jambo mbele ya Waandishi wa Habari katika mapokezi ya majokofu ya kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa katika vituo vya Afya hapa nchini, yaliyofanywa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (wakatikati) tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. (kushoto) Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi,
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu   akipokea majokofu ya kutunzia chanjo, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung (Watatu kushoto)  tukio limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Kulia kwa Waziri Ummy ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhammad Bakari Kambi, na Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.
Muonekane wa majokofu ya kutunzia chanjo, kutoka yaliyotolewa na Mkuu wa Masuala ya Afya UNICEF Kyaw Aung.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


Hivyo makala SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO

yaani makala yote SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/serikali-yawaasa-wananchi-kuwapeleka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO"

Post a Comment

Loading...