Loading...
title : TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO
link : TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO
TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua rasmi kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akiwakaribisha katika mkoa wake wajumbe wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge wakati wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dkt. Jabiri Bakari akizungumza kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.

Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Taasisi serikalini wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma mapema leo.
………………………..
Taasisi za Umma nchini zimetakiwa kuzingatia viwango vya usalama wakati wa uundaji wa mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma ili kukabiliana na changamoto ya usalama wa taarifa za serikali mitandaoni.
Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini chenye lengo la kubadilishana uzoefu, kujenga uelewa wa pamoja na kuendeleza uhusiano katika utendaji kazi na wadau mbalimbali wa Serikali Mtandao.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, suala la usalama mitandaoni lisipokabiliwa kikamilifu, linaathiri kwa kiasi kikubwa jitihada za serikali zilizofanyika katika eneo la Serikali Mtandao na kuongeza kuwa tatizo la usalama mitandaoni linazidi kukua kadri maendeleo ya teknolojia yanavyozidi kukua.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, usalama wa taarifa za serikali liwe jambo la kwanza na la lazima wakati wa kubuni, kusanifu, kujenga, kusimika na kuendesha mifumo ya TEHAMA badala ya kujenga mifumo hiyo kwanza na ndio suala la usalama lifuate.
“Njia mojawapo ya kuhakikisha usalama, ni kuhakikisha utengenezaji wa mifumo yetu unazingatia programu ambazo wataalamu wetu wanaweza wakatambua kinachofanyika badala ya kuwa na mifumo ambayo hatujui kinachoendelea nyuma ya pazia,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amezihimiza taasisi zote za umma kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao iliyowekwa na inayoendelea kuwekwa ili kuhakikisha matumizi sahihi ya TEHAMA ndani ya Utumishi wa Umma.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, iwapo utekelezaji wa mifumo na miundombinu ya TEHAMA utawianishwa na kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa ndani ya taasisi za umma na baina ya taasisi za umma, ni dhahiri kuwa utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao utakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo ya viwanda ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuyapata.
Serikali imedhamiria kuimarisha miundo mbinu ya TEHAMA, uratibu wa shughuli za TEHAMA na usalama wa taarifa za Serikali ili kuongeza ufanisi katika sekta ya umma, kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za serikali na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hivyo makala TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO
yaani makala yote TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/taasisi-za-umma-zatakiwa-kuzingatia.html
0 Response to "TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO"
Post a Comment