Loading...
title : TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA
link : TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA
TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imefunguka rasmi kuwa itatangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga ifikapo machi 5 mwaka huu. Hiyo ni baada ya kamati hiyo kukaa kimya kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo iliyokita maskani yake Jangwani maeneo ya Kariakoo Jijini Dar Da Salaam.
Amesema hayo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Ally Mchunguhela kuwa tayari ameshakutana na viongozi wa klabu ya Yanga na kukubaliana kuwa sasa kinachosuburiwa ni kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa klabu hiyo.
Mchungahela amesema kuwa uchaguzi huo ulipaswa kufanyika januari 13 mwaka huu lakini kutokana na baadhi ya wanachama wa Yanga kufungua kesi mahakamani kusimamisha mchakato huo na kupelekea zoezi zima la uchaguzi kusimama.
"Uchaguzi wa Yanga utafanyika na hakutakuwa tena na mchakato mwingine mpya bali utaendelea palepale ulipokuwa umefikia ,na ifikapo Tarehe 5 Machi tutatangaza rasmi tarehe mpya ya uchaguzi wa Yanga na naamini utafanyika",amesema mchungahela.
Aidha Mchungahela amesema kuwa mpaka kufikia tarehe itakayotangazwa rasmi ya uchaguzi huo kila kitu kitakwenda sawa na hakutakuwa tena na kizuizi kingine ambacho kitafanya mchakato mzima kusimama.
Hivyo makala TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA
yaani makala yote TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/tff-ifikapo-machi-5-tutangaza-rasmi.html
0 Response to "TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA"
Post a Comment