Loading...
title : TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti.
link : TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti.
TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti.
Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein kulia akizungumza na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kushoto wakati wa ziara yake kwa walipakodi wanaotumia mashine na EFD na wasiokuwa nazo ili kubaini changamoto na kuziboresha
Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein kulia akizungumza na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kushoto wakati walipoingia kwenye duka hilo
Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein kulia akimuonyesha Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure namna wanavyotumia mfumo wa EFD Mashine kutoka huduma zao kwa wateja wao kushoto wakati walipoingia kwenye duka hilo
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akimuonyesha Mfanyabiashara Yusuph Tayabani kitu kwenye risiti wakati wa ziara hiyo
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akitoka kwenye mmoja ya duka ambalo alilitembelea wakati alipowatembelea walipakodi wanaotumia mashine na EFD na wasiokuwa nazo ili kubaini changamoto na kuziboresha
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure katikati akiwa na maafisa wengine wa TRA mkoani Tanga wakitoka kwa duka la kuuzia gesi wakati wa ziara hiyo
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure |
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) Mkoani Tanga wamefanya ziara ya kutembelea walipakodi waliokuwa na mashine za EFD na wasiokuwa nazo ili kuweza kubaini changamoto zao na kuweza kuboresha huduma zao.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa TRA Mkoani Tanga Specioza Owure alisema baada ya kutembelea walipakodi hao wameona wapo walikuwa wanastahili kuwa na mashine za EFD lakini hawana hivyo kuwaachia barua za kwenda kununua mashine hizo.
Alisema pia wamelazimika kutoa barua za wito kwa baadhi yao ili waweza kufika ofisi za mamlaka hiyo kwa ajili ya kuona kumbukumbu za mauzo na manunuzi ili kuona kama wanastahili kwa na mashine za EFD
Meneja huyo alisema kwamba ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kuendelea kutumia mashinde za EFD ikiwemo kuwataka wanunuzi nao kudai risiti wakati wanapofanya manunuzi.
“Lakini pia tumewaelimisha walipa kodi athari za kutokutoa risiti na kutokutumia mashine za EFD na kwamba usipotoa risiti adhabu yake ni milioni tatu mpaka nne na nusu huku kwa wale wasiodai risiti adhabu yake inaanzia elfu 30 hadi milioni 1.5 au kifungo kisichozidi miaka mitano”Alisema.
Awali akizungumza katika ziara hiyo Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein alisema umuhimu wa mashine hizo ni mkubwa kwani unarahisisha kufahamu mauzo ya siku na pia kuchangia maendeleo ya nchi .
Hussein alisema pia mfumo huo unawafanya wafanyabiashara kutokuibiwa kutokana na kila anayenunua bidhaa anapata risiti na hivyo kuwa rahisi kuweza kujua mauzo ya siku husika lakini pia kuchangia maendeleo ya nchi.
Hata hivyo alisema kwamba changamoto kubwa ambayo wanakumbana n ayo ni mtandao wa hizo mashine wakati mwengine unasumbua lakini pia ni ghali sana inabidi wapunguze maeneo ya mauzo yao unatakiwa ununua sita au zaidi ya hapo kama utaboreshwa mfumo vizuri unawasaidia kuweza kutambua mauzo.
Mamlaka hiyo iliwatembelea maduka mbalimbali yakiwemo ya dawa,vituo cha kuuzia mafuta cha Ratco,Super Marketi ya Mkwabi na maduka ya kuuza bidhaa za jumla za vyakula.
Hivyo makala TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti.
yaani makala yote TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/tra-tanga-yawataka-wafanyabiashara_17.html
0 Response to "TRA Tanga Yawataka Wafanyabiashara Kutumia Mashine za EFD,Wanunuzi Nao Watakiwa Kudai Risiti."
Post a Comment