Loading...

VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA

Loading...
VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA
link : VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA

soma pia


VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana mkoani Kigoma waanzishe mashamba ya michikichi kwa kuwa zao hilo litawapatia kipato cha uhakika. Amesema Serikari imedhamiria kufufua zao la michikichi ili kuliwezesha Taifa kujitosheleza kwenye mafuta ya kula na kuokoa fedha za kigeni.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 18, 2019) alipowasalimia wananchi wa kijiji cha Nyakitondo wilayani Kasulu akiwa njiani kwenda Kibondo.
Waziri Mkuu ambaye yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kufufua kilimo cha michikichi amesema ni vema wananchi wakachangamkia fursa hiyo.

“Vijana limeni michikichi kwani ukipanda ukiwa darasa la tano baada ya miaka mitatu utaanza kuvuna na kujipatia kipato ambacho kitakuwezesha kujikimu.” Amesema kilimo cha zao la michikichi kitawawezesha wananchi hususani vijana kupata mitaji ya uhakika kwa ajili ya shughuli zingine za kiuchumi

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania inaongoza kwa kilimo cha zao la michikichi katika nchi za Afrika Mashariki. Kadhalika, Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi hao wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili wawe na uhakika wa matibabu kwa yao na familia zao.
Wakati huohuo Waziri Mkuu ametembelea kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo na kukagua shule ya msingi Kassim Majaliwa na baadae wodi ya wazazi katika Hospitali Nduta.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye moja ya madarasa katika Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa iliyopo kwenye  Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua madaftari ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa wakati alipotembelea baadhi ya madarasa ya  Shule hiyo, Februari 18, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watoto wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa  wakati alipokagua madarasa ya Shule hiyo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Kibao kinachoonesha ilipo Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa  katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo ambayo ilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Hivyo makala VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA

yaani makala yote VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/vijana-anzisheni-mashamba-ya-michikichi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...