Loading...

Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho

Loading...
Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho
link : Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho

soma pia


Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho

Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma  imeanza kufanya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya macho katika kambi maalum iliyoanza tarehe18-2-2019 katika hospitali hiyo na wagonjwa zaidi ya 500 wameshaonwa na mpaka sasa wagonjwa 150 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao ni nzuri.

Hayo yalibainishwa na Daktari bingwa wa macho Dk.Frank Sandi wa Hospitali hiyo alipokuwa akizungumzia kuhusu kambi hiyo. "Katika upasuaji wa macho uliofanyika watu wengi waliojitokeza wameonekana kusumbuliwa na matatizo ya mtoto wa jicho na Trakoma kutokana na kuugua mara kwa mara na sababu kubwa ni kutokuosha nyuso zao vizuri”, alisema.

 Dkt. Frank Sandi alisisitiza kuwa tatizo la macho ni kubwa na linatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuyaweka macho katika hali ya usafi pamoja na kuyakinga na mazingira hatarishi yanayoweza kujeruhi ikiwemo upasauaji wa kuni. “Kati ya wagonjwa waliokuja katibiwa, asilimia 30 ya wagonjwa wamebainika kuwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho, na wachache wenye ugonjwa wa vikope (trakoma),”alisema.

 Hata hivyo Dkt Frank alisema kwamba magonjwa mengine yaliyogundulika katika uchunguzi unaoendelea ni pamoja na ugonjwa wa kutoona vizuri na majeraha kwenye macho. “Baadhi ya wagonjwa tuliowaona hapa wameonekana kuwa matatizo ya uoni pamoja na majeraha yanayotokana na kurukiwa na vitu kwenye macho,”alisema. Madhumuni ya kambi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka hospitalini hapo kwa kushirikiana na wadau kutoka Marekani ni kutoa huduma za macho kwa wananchi wanaoishi kwenye mazingira ambayo si rahisi kufikika. Na lengo lao mwaka huu ni kuwafikia watu wasiopungua 1,500 na kati yao zaidi ya wagonjwa 400 watafanyiwa upasuaji.

“Hadi sasa tumeshawaona wagonjwa 400 na kati yao, wagonjwa 150 wameshafanyiwa upasuaji. Tunaendelea kutoa huduma za macho kila siku hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma hii,” alisema. Naye, Mkazi wa Chimendeli Marta Nhuguti mwenye umri wa miaka 110 aliishukuru hospitali hiyo kwa kutoa huduma hiyo na kudai kuwa alikuwa haoni lakini sasa anaona.
 Madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na wenzao wa Chuo cha Utah kilichopo Marekani wakifanya uchunguzi na upasuaji wa macho yenye uoni hafifu, mtoto wa jicho na majeraha.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa, Frank Sandi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye kambi maalum ya tiba kwa wagonjwa wa macho inayofanyika kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho , Frank Sandi akimuonesha   Bi.Martha Nhuguti ishara ya vidole ili kuthibitisha kama anaona vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho katika kambi maalum inayofanyika kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Uchunguzi wa macho ukiendelea  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa


Hivyo makala Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho

yaani makala yote Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/wagonjwa-zaidi-400-kufanyiwa-upasuaji.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wagonjwa zaidi 400 kufanyiwa upasuaji wa Macho"

Post a Comment

Loading...